ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 31, 2016

KAMATI YA BUNGE, MALIASILI, UTALII, ARDHI NA MAZINGIRA WAMTAKA WAZIRI LUKUVI KUFUTA HATI MILIKI YA ECO ENERGY

 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Injinia Ramo Makani kulia akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili,Ardhi na Utalii,Meja Jenerali Gaudance Milanzi katikati kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa wa Shirika la Hifadhi za Taifa(TANAPA), Ibrahim Mussa wakati wa ziara ya siku moja ya kamati ya Bunge Maliasili,Ardhi na Utalii kwenye hifadhi ya Taifa ya Saadani,
Wajumbe wa Kamati ya Bunge,Maliasili, Ardhi na Utalii wakiingia kwenye hifadhi ya Taifa ya Saadani jana.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge,Maliasili,Ardhi na Utalii Atashasta Justus Nditiye akitoa maazimio ya kamati hiyo mara baada ya kuitembelea hifadhi ya Taifa ya Sadani wa kwanza kushoto ni Mjumbe wa kamati hiyo,Marry Chatanda ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe mjini.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Injia Ramo Makani akizungumza wakati wa ziara hiyo
Kaimu Mkurugenzi wa (TANAPA),Ibrahim Mussa akizungumza wakati za ziara ya kamati ya Bunge Maliasili,Utalii na Ardhi Mazingira ilipotembelea hifadhi ya Taifa ya Saadani.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Meja Jenerali Gaudance Milanzi akizungumza wakati za ziara ya siku moja ya Kamati ya Bunge ya Maliasili,Utalii na Ardhi
 Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Tanapa,Mtango Mtaniko akizungumza wakati wa ziara ya kamati ya Bunge Maliasili,Utalii na Ardhi walipofanya ziara ya kutembelea hifadhi ya Taifa ya Saadani
Mjumbe wa Kamati ya Bunge Maliasili,Utalii,Ardhi na Mazingira,Pauline Gekule akiulizwa swali wakati ziara hiyo
MJUMBE wa Kamati ya Bunge,Maliasili,Ardhi na Utalii,Shabani Shekilindi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Lushoto mkoani Tanga akiuliza swali wakati wa ziara hiyo
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini,Marry Chatanda ambaye pia  ni mjumbe wa kamati hiyo akichangia hoja kwenye ziara hiyo

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudance Milanzi kulia akiteta jambo na Meneja wa Mawasiliano wa Tanapa,Pascal Shelutete wakati kamati ya Bunge Maliasili,Ardhi na Utalii walipotembelea hifadhi ya Taifa ya Saadani Picha kwa Hisani ya Tanga Raha Blog

1 comment:

Anonymous said...

Ndugu mwenyekiti wa kamati ya bunge ya maliasili,Tunaiomba sana kamati yako itufanyie uchunguzi wa waziri wa maliasili na utalii Bwana Magembe,kwa kufanya maamuzi ambayo hata hakufanyia uchunguzi wa kusimamisha biashara ya viumbe hai bila kufuata taratibu,eti kwa kisingizio cha tumbili wanaotoroshwa.sasa imethibitika kuwa yeye kapigiwa simu na mfanya biashara mmoja wa wa kirusi hapa dar es salaam (ambaye ana leseni ya nyara hapa Tanzania) kuwa kuna tumbili wanatoroshwa na hawana vibali bila kufanya uchunguzi ukweli huyu mrusi baada ya kukosa soko la kuuza hao ngedere kwa waholanzi ndio walioshinda tenda Armenia (waliokamtwa) ya kuuza hao ngedere kaamua kuwafanyia fitina kwa kueneza habari za uongo kuwa hawa jamaa hawana vibali wakati wanakila kitu,je waziri anawezaje kumsikiliza mtu tena mfanya biashara binafsi bila kufanya uchunguzi wa kuwashilikisha wataalamu wa wizara yake??? je hawa ndiyo mawaziri wa magufuli wanaokulupuka tu bila kufanya uchunguzi na kujichukulia sheria za kibabe siyo kuwatumikia wananchi walioplipia vibali na bila taarifa anaamua anavyotaka.hii serikali ya wapi isiyofuata sheria mtu anaamua tu