Na Mauwa Mohammed Zanzibar
IDADI ya viongozi wa chama cha wananchi CUF kohojiwa na kushikiliwa na Jeshi la Polisi imeongezeka baada ya aliyekuwa mshauri mgombea chama katika uchaguzi uliopita katika mambo ya siasa wa chama hicho Mansoor Yussuf Himid kwa mahojiano kuhusiana na kulipuliwa kwa maskani ya CCM, Kisonge Michenzani mjini Unguja.
Katibu Mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazrui alisema kuwa kiongozi wao Mansoor Yussuf Himid alipokea wito mchana wa jana uliomtaka aende kituo cha Polisi madema kwa ajilili mahojiano na kudai kwamba kushangwazwa kawekwa ndani.
Kufuatia kadhi hiyo Mazrui ameliomba jeshi la Polisi kutofanya upendeleo na kuegemea upande mmoja katika kutekeleza majukumu yake ya kulinda raia na mali zao.
“Haya ni maonevu makubwa kwani kila uchao tunakamatwa sisi tuu bila kujua kosa letu lakini sishangai sana ndio utawala wa kibabe huu” alisema Mazurui.
Alisema matukio haya yamekuwa yakiendelea kwani juzi ofisi zachama zilioko Mpendae zilivamiwa na kuchukuliwa wananchama wao 30 bila kujua wale wamo katika maeneo yao.
“Wametuvamia katika ofisi halafu wakaharibu kwa kuzichana nyaraka zetu muhimu sanaa, mhh hatujui hawana wanalengo gani kwa kweli” alillalama Mazurui
Alisema kuwa mara baada ya kutokea tukio hilo CUF tayari imeanza kuchukua hatua mbadala ikiwemo kuripoti katika jeshi hilo ili kuweza kujua tuhuma zinazowakabili wanachama hao.
Alisema kuwa katika tukio hilo ambapo baadhi ya vifaa vilivyokuwemo katika ofisi hiyo ikiwemo computer, mashine ya kutolewa fotokopi viliharibiwa vibaya pamoja na upotevu wa pesa.
CHANZO: HABARI MSETO BLOG
CHANZO: HABARI MSETO BLOG
No comments:
Post a Comment