kushoto meneja mkuu wa kiwanda cha maziwa cha tanga fresh Bw. Michael Kalata, akimuonyesha mh Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Luhaga Mpina, moja nya bidhaa ya maziwa inayozaliswa katika kiwanda hicho. mh Mpina alitembelea baadhi ya viwanda jijini tanga kujionea namna ambavyo vinatekeleza sheria ya mazingira ya 2004 na kanuni zake.
Pichani Namna ambavyo fukwe ya Pangani Jijini Tanga ilivyoliwa na maji ya bahari, kutokana na kuongezeka kwa kina cha bahari ikiwa ni athari zitokanazo na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi. na baaadhi ya visiwa nchini viko hatarini kumezwa na bahari.
Mh Luhaga Mpina Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira aliyea nguo nyeusi akipata maelezo toka kwa mtaalam katika kiwanda cha Twiga cement alipokitembelea leo jijini tanga kuona namna ambavyo kiwanda hicho kinatekeleza sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake. (Picha zote na Evelyn Mkokoi wa Ofisi ya Makamu wa Raisi)
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh Luhaga Mpina akitolea ufafanuzi namna ambayo fukwe ya Pangani imeathirika na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh.
Luhaga Mpina (MB) amekifungia kiwanda cha kuzalisha cement na chokaa
kilichopo jijini Tanga cha Rhino Cement, leo
jioni kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni uharibu na uchafuzi wa
mazingira na kuvunja sheria ya usimamizi wa mazingira ya mwaka 2004 na
kanuni zake.
Mh.
Mpina amechukua uamuzi huo, baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa
wananchi wa kata ya maweni kupitia diwani wa kata hiyo Bw. Joseph Colvas
na kujionea mwenyewe namna ambavyo kiwanda hicho kinavyo achilia moshi
mzito kwenda angani, pamoja na vumbi lisilovumilika kusambaa katika
maeneo ya makazi ya wanachi wa kata hiyo ikiwa ni pamoja na kusambaa
katika maeneo ya shule ya sekondari ya Don Bosco ambapo, Mh. Mpina
ameelezwa kuwa athari zitokanazo na uachiachi wa hewa hiyo chafu angani
si tu kwa watoto wa shule zinazozunguka kata hiyo bali pia ni kwa viumbe
hai na mazingira.
“Hawa
jamaa wamekuwa wakiachilia vumbi jingi na moshi mzito kutoka katika
kiwanda hiki mara kwa mara, hivi tangu jana wamezima mitambo yao wakijua
kabisa kuwa kuna ugeni wa Naibu Waziri kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais,
Alisisitiza Bw. Joseph.”
Kwa
upande wake Afisa Afya wa jiji la tanga aliyejulikana kwa jina moja la
bwana Kizito alimuelezea Naibu Waziri Mpina kuwa ni kweli kiwanda hicho
kimekuwa kikifanya uchafuzi huo wa mazingira, na Afisa uendeshaji kutoka
Baraza la Taifa na HIfadhi ya Mazingira NEMC Bw. Novatus Mushi ameeleza
kuwa kiwanda hicho kimeshawahi kutozwa faini ya shilingi milioni kumi
na saba (17) kwa kosa la kuchelewa kulipa ada ya mwaka ya mazingira
pamoja na uharibifu wa mazingira uliokuwa ukifanywa na kiwanda hicho kwa
upande wa kuzalisha chokaa.
Mh.
Mpina ameelekeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (
NEMC) kukifunga kiwanda hicho kisiendelee na uzalishaji kwa muda
usiopungua miezi mitatu, na kulitaka baraza hilo lijiridhishe na
kufuatilia namna kiwanda hicho kinavyotakiwa kutekeleza sheria ya
mazingira kwa kujenga mfumo wa kisasa wa kutoa taka zitokanazo na
uzalishaji kiwandani hapo pamoja, na kupima vumbi na moshi utokao
kiwandani hapo kama hautakuwa na madhara na athari kwa mazingira na
viumbe hai. Kinyume na hapo kiwanda hicho kitafungiwa moja kwa moja.
Aidha,
akitolea mfano wa kiwanda cha bonite bottles cha mjini moshi kwa kuwa
kinara katika upandaji miti na utunzaji wa mazingira, mh Mpina alivitaka
viwanda vingine viige mfano wa kiwanda hicho cha coke cola.
Ziara
ya Mh. Mpina Jijini Tanga ilihusisha pia kuangalia namna ukuta wa fukwe
ya Pangani uliojengwa enzi za mkoloni, ulivyo athirika na madhara
yatokanayo na athari za mabadiliko ya tabia nchi na kusema kuwa, ukuta
huo huko kwenye mchakato wa kujengwa na kuboreshwa upya, ifikapo mwezi
wa nne mwaka huu mradi wa
ujenzi wa ukuta huo utaanza kutekelezeka kwa kuwa tenda imeshatangazwa
na jumla ya kiasi cha fedha za kimarekani dola milioni 1,400
zimepatikana kupitia mfuko wa nchi maskini zaidi duniani (LDCf).
Mh.
Mpina aliwaasa wakazi wa mji wa Tanga na viunga vyake kutunza mazingira
kwa kupanda miti na kufanya usafi kama ilivyoagizwa na serikali, ili
kuhepukana na nchi kuwa janga na magonjwa yatokanayo na uchafu. Waziri
Mpina Pia alitembelea kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh na kiwanda cha
Tanga Cement na kuridhirishwa na namna ambayo wanatekeleza sheria ya
mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake.
No comments:
Post a Comment