Advertisements

Friday, March 4, 2016

MAZISHI YA MAMA YAKE MZAZI ANGEL AKILIMALI

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiwa kwenye ibada ya kumuombea marehemu Mama Celina Akilimali kwenye kanisa katoliki la Chang'ombe .
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Mama Celina Mfala Akilimali ambaye ni mama wa Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM Bi. Angel Akilimali kwenye kanisa katoliki la Chang'ombe .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa pamoja na Mwenyekiti wa bodi ya Uhuru Media Alhaji Adam Kimbisa kwenye makaburi ya kinondoni wakati wa mazishi ya Mama Celina Mfala Akilimali ambaye ni mama mzazi wa Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM B. Angela Akilimali.
Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM Bi. Angel Akilimali (kushoto)akiwa na mtoto wake pamoja na mumewe wakiweka udongo kwenye kaburi la mama yake marehemu Celina Akilimali.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Celina Akilimali mama mzazi wa Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM Bi. Angel Akilimali.
Mwenyekiti wa bodi ya Uhuru Alhaji Adam Kimbisa akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Celina Mfala Akilimali , mama mzazi wa Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongea na watangazaji wa radio Uhuru FM waliojitokeza kwenye mazishi ya mama Celina Akilimali, mama wa Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali kwenye makaburi ya kinondoni jijini Dar es Salaam.

No comments: