ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 14, 2016

Mbowe atoboa siri uteuzi Dk. Mashinji

mashinji
Na Fredrick Katulanda, Mwanza

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ametoboa siri ya kumteua Dk. Vincet Mashinji kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho.

Mbowe alisema amemteua Dk. Mashinji kutokana na kiwango chaka cha elimu pamoja na ushujaa wake wa kupambania maslahi ya madaktari kwa kuitisha migomo.

Akihutubia maelefu ya wakazi wa Jiji la Mwanza jana katika viwanja vya Furahisha wakati wa kumtambulisha kiongozi huyo, Mbowe alisema Chadema imemteua Dk. Mashinji kutokana na sifa, uwezo na si kwa sababu ya ukabila.

Alisema kwa uteuzi huo, ametoa somo kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuteua mtu ambaye baba yake si kigogo wa chama, tofauti na wao ambao wamekuwa wakitoa nafasi kwa watoto wa vigogo au kwa misingi ya rushwa.

Alisema Dk. Mashinji ana kiwango cha juu cha elimu na si mwoga jambo ambalo anaamini litamsaidia kuendesha chama.

“Baada ya kupekuwa historia yake tulibaini ni mmoja wa wale walioanzisha mgomo wa madaktari nchi nzima, kisha akafukuzwa akiwa na wenzake kina Dk. Steven Ulimboka.

“Tulipogundua aliongoza mgomo tulijua si mwoga, kama alikomaa kutetea maslahi ya madaktari na wenzake, basi tuliona anafaa kukomaa kutetea Watanzania… si mtoto wa Mbowe wala mtoto wa Lowassa (Edward).

“Tumeamua kumteua mtu mwenye sifa na uwezo pamoja na karama za uongozi, tumemwibua kutoka chini, angekuwa CCM angelazimika kuhonga mpaka ndugu zake ili ashinde nafasi hii,” alisema.

Alisema uteuzi huo, unaonyesha dhamira ya Chadema ya kugawana madaraka na kubainisha ndani ya Kamati Kuu wapo watu ambao wana sifa za kuwa makatibu wakuu, lakini wana majukumu mengine.

Alisema wamekubaliana walioko bungeni waendele kupambana huko ili mambo mengine yafanywe na katibu.

Dk. Mashinji

Kwa upande wake, Dk. Mashinji akizungumza baada ya kutambulishwa, alisema jukumu la kwanza ambalo linamkabili ni kujenga chama hicho kimkakati.

Alisema atafanya kazi zake kisasa kwa lengo la kuongeza ufanisi.

Alisema tayari ametoa maelekezo kwa madiwani wa Chadema katika halmshauri zote kuanza kuunda kamati za ufuatiliaji za wananchi ambazo zitakua na jukumu la kufuatilia utendaji na utekelezaji na maendeleo kwa kata husika.

“Huu ndiyo mkakati wangu wa kwanza naanza kuutoa hapa, umebeba lengo la la kuisukuma Chadema mbele na kufanikisha kushinda na kushika dola mwaka 2020.

Lowassa

Kwa upande wake, aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya chama hicho, Edward Lowassa aliwashukuru wananchi wa Mwanza kwa kumpigia kura wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka jana.

Alisema kura nyingi alizopata ni kielelezo cha kukubalika kwa wananchi hao, japokuwa waliotangaza walisema hazikutosha.

Alisema imani yake ni kujipanga zaidi ili mwaka 2020 washike dola na kwamba wamepata katibu mkuu mpya kijana ambaye atasimamia chama vilivyo na anaamini watafanya vizuri zaidi.

Wenje

Akizungumzia uchaguzi, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Ezekiel Wenje alisema kulingana na matokeo yalivyo, japo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), haikumtangaza anatambua yeye ndiye mshindi na ndiyo maana amekwenda mahakamani kufungua kesi.

Aliomba wafuasi wa chama hicho kumwombea, wakati huu ambao kesi yake inaendelea kusikilizwa mahakamani.

“Ukitaka kujua nani kashinda tupite mtaani mimi na huyo Mbunge wa CCM (Stanslaus Mabula), utaona yeye anatembea na polisi, mimi napita nakatiza mitaa, hii maana yake aliyetangazwa anatembea na hofu ya Mungu,” alisema.

Mwalimu

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar ) Salum Mwalimu alisema uteuzi wa Dk. Mashinji umeonyesha ukomavu ndani ya chama na namna ambavyo inaweza kuibua watu wenye karama za uongozi.

“Niseme CCM imezoea kununua watu wa upinzani, kila ikinunua sisi tutaibua wapya kama tulivyofanya kwa Dk. Mashinji,” alisema.

MTANZANIA

3 comments:

Anonymous said...

Kila mtu anaamimi yeye ndiye aliyashinda; urais, ubunge, udiwani etc. Hata Mimi naamini nilishinda urais ila Tume haikunitangaza tu!


Kama kuitisha migomo ni sifa ya uongozi badi kweli sasa tunakwenda kipindi cha Hapa Kazi tu!

Anonymous said...

Kwa viongozi wa chadema kujisifia kuwa imemchagua katibu mkuu wa chama chao kwa sifa ya kuwa muumini mzuri wa vurugu, maandamano na migomo ni jipu na upotofu uliotukuka kabisa. Na hii inaonesha dhahiri yakwamba chadema ni chama kinachoabudu vurugu kama moja ya sera yao kuu ya kuendesha chama chao. Na hiyo ya kusema yakwamba wamechagua katibu wao mkuu si kwa misingi ya ukabila ni porojo za hovyo kwani asiejua yakwamba CCM haina mwenyewe Tanzania,isipokuwa wenyewe ni watanzania tofauti na chadema kila mtanzania anaju chama hicho wenyewe ni watu wa kaskazini mwa Tanzania naomba samahani kama kutakuwa na watu nimewakwaza lakini msema kweli ni kipenzi cha Mungu, na hakuna cha kusema yakwamba kaskazini mwa Tanzania ni strong hold ya chadema wala nini bali ukweli ni kwamba kaskazini mwa Tanzania ni ethnic majority of chadema party. Huyo msukuma kawekwa hapo kama mizunguo tu yaanu funika kombe mwanaharamu apite na zaidi nathubutu kusema ni ukabila wake ndio kigezo kikubwa kilicho mpa sifa ya kupata hiyo nafasi . Ukichunguza kwa makini kwa chadema kumchagua huyo ndugu mashinji wamelenga katika kujikita katika ukabila zaidi tofauti na porojo zao za kujidai wao ni watu wa kutizama uwezo wa mtu wa elimu. Zito Kabwe ni msomi,smart,kijana na kakulia ndani ya chama na anaijua chadema kuliko hata Mbowe kwanini katimuliwa? Zito alikuwa anapigania usawa ndani ya chadema akasukiwa zengwe la ajabu ili upatikane uhalali wa kumtimuwa ndani ya chama lakini waswahili wanasema vya watu haviliwi vitakudhuru tu.Hata hivyo zito anatoka kigoma ni kigoma tu sio mwanza,shinyanga,geita,tabora na hata kagera ni mikoa iliokusanya karibu watanzania wenye tamaduni karibu ya aina moja kwa hivyo utaona kwa chadema kumchagua kiongozi wao chama hapa ni sehemu muafaka kabisa katika kuendeleza kasumba yao ya ukabila. Mfano chama cha mapinduzi. Mwenyekiti wao wa chama anatoka Bagamoyo. Makamo mwenyekiti sina uhakika nadhani anatoka Zanzibar. Katibu mkuu wao anatoka Arusha. Msaidizi wake anatoka Lindi. Raisi alietokana na chama cha mapinduzi anatoka Kato sijui shinyanga nisipokujua mimi. Hakika CCM ni mfano wa kuigwa na kila taasisi za siasa katika kila nchi barani Africa kuhakikisha zinawaunganisha raia wake bila ya kujali tofauti zao kutokana, na udini ukabila,urangi,ujimbo kama ilivyo kwa CCM Tanzania basi Africa ingekuwa sehemu salama sana ya kuishi hapa duniani,myonge mnyongeni lakini haki yake msiisahau. Ati halafu kiongozi mkubwa wa chadema anathubutu kuropokwa yakwamba CCM imezoea kununua viongozi kutoka upizani? Hivyo ni vichekesho vya karne. CCM kweli inashida ya viongozi hadi kwenda kununua wa upizani? Hao upinzani viongozi wamewatengeneza lini kama hawatoki CCM? Huyo Mbowe na hao waliomuweka hapo alipo wote walikuwa CCM. Huyo Lowasa katoka wapi? Lipumba katokea wapi? Seifu sharif katokea wapi? Chadema kujilinganisha na CCM ni sawa na TOTO FC ya mwanza kujilinganisha na Azam ya Baharesa. Watanzania wanaweza kuwasapoti Chadema tena kwa idadi kubwa tu lakini isiwe sababu ya kuvimba kichwa na kujifananisha na CCM katika misingi ya kiutawala chadema bado tena sana na wala hamtakiwi kwenda nje kujifunza siasa kwani hiyo hiyo CCM ni mwalimu wenu tosha kabisa kama mtaachana na upuuzi wenu wa kujifanya mnajua

Anonymous said...

Zitto tapeli mnafiki na mbinafsi