NA
K-VIS MEDIA/Khalfan Said
POLISI
wamelazimika kufyatua mabomu ya machozi kuwatawanya watu waliojikusanya mbele
ya Benki ya CRDB tawi la Mbagala-Rangi Tatu, baada ya mtu mmoja aliyekuwa
akiongea na simu ndani ya benki hiyo kukaidi maagizo ya polisi ya kuacha
kufanya hivyo mapema leo mchana Machi 11, 2016.
Kwa
mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, watu watatu mmoja akiongea na simu na
wengine wawili waki-chat, ndani ya benki hiyo, waliagizwa na mlizni wa benki
kuacha kufanya hivyo lakini wakakaidi.
Baada
ya mlizni kuona hivyo alitoa taarifa kituocha polisi Mbagala-Maturubai, nahapo
polisi wakiwa ndani ya gari lao maarufu kama Defender, waliwasili kwenye eneo
hilo na kuamuru watu hao ambao wanaelezwa kuwa wateja, kutoka ndani ya benki
hiyo.
Hata
hivyo palitokea mabishanobaadaya mmoja wao kukaidi amri ya polisi na kuanza
kupigana nao.
Kuona
hivyo wtu walianza kujaa na polisi bila kufanyaajizi wakafyatua mabomuya
machozi kutawanya watu na kuwadhibiti “wateja’hao wabishi na hatimaye
kufanikiwa kuondoka nao.
Hali
hiyo ilizua tafrani hadi watu wakadhani kuwa palikuwepo na tukio la ujambazi
kwani ni mwezi uliopita umbali wa mita chache kutoka kwenye benki hiyo,
palitokea tukio baya ya uvamizi wa benkiya Access ambapo watus aba waliauawa
wakiwemo polisi.
No comments:
Post a Comment