Mkuu
mpya wa Mkoa wa Kagera,Meja Jenerali Mstaafu,
Salum Kijuu amewaagiza watumishi wasio na sifa za
kuajiriwa kujiondoa kabla ya March 31 mwaka huu.
Kijuu
alitoa kauli hiyo jana wakati wa
Makabidhiano ya ofisi baina yake na mkuu
wa mkoa wa zamani,John Mongella ambapo alisema
kwamba Tanzania inawatumishi hewa zaidi ya 2000,
hivyo ana imani hata Kagera wapo.
"Hao
watumishi hewa endapo watang'ang'ania kubaki katika
vitengo walivyopo nitawashughulikia wahusika wakuu
wa vitengo hivyo," alisema
Aidha,
aliagiza wakuu wote wa wilaya za mkoa huo kusimamia uundwaji wa mabaraza
ya usuluhishi kuanzia ngazi za kata hadi mkoa ili
kusimamia haki za wananchi.
Pia
aliwataka watumishi wa serikali mkoani humo
kufahamu maudhui ya "Hapa Kazi Tu", kwa kufanya kazi kwa kasi,haraka,
nguvu, maarifa na uadilifu.
Aliwataka
kutosubiri kusukumwa, lakini wajitambue wao ni akina nani na
wanapaswa kufanya nini kutokana na majukumu
waliyopewa.
Alisema
ili kufikia lengo la Rais John Magufuli la kuwatumikia
wananchi kwa uaminifu ni lazima kushikiria
uadilifu na kutambua kwamba watumishi wapo kwa ajili ya kutoa
huduma kwa jamii.
No comments:
Post a Comment