ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, March 8, 2016

SERIKALI YATANGAZA BEI MPYA YA SUKARI NCHI NZIMA

Siku chache baada ya Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutangaza zuio la uingizwaji wa bidhaa ya sukari kutoka nje ya nchi, leo March 8 2016 Serikali kupitia bodi ya sukari Tanzania, imetangaza viwango vipya vya bei ya sukari nchini vitakavyoanza kutumika hivi karibuni, akiongea na waandishi wa habari Mkurugenzi wa bodi ya sukari Tanzania Henry Semwanza amesema.

Serikali, kupitia bodi ya Sukari Tanzania, inawaarifu wananchi wote kuwa bei ya rejareja ya sukari sasa itakuwa sh. 1,800 kwa kilo moja‘

‘wafanyabiashara wote wanapaswa kuzingatia agizo hili, pamoja na kuhakikisha kuwa sukari inaendelea kusambazwa na kuuzwa kwa wananchi bila kuihodhi‘

‘Maafisa biashara wa mikoa na wilaya watafuatilia na kusimamia utekelezaji wa agizo kuhusu bei elekezi ya sukari, na hawatasita kuchukua hatua stahiki za kisheria kwa wale watakaobainika kupandisha bei ya bidhaa hiyo‘

2 comments:

Anonymous said...

Hivi mbona kama tumerudi kwenye enzi za "mgao" kipindi cha mwisho cha utawala wa Mwalimu!! Nilidhani tumepiga hatua kwenda na upepo wa kibiashara duniani na tupo kwenye zama za masoko huria. Sasa hivi unapopanga bei moja ya kilo ya sukari kwa nchi nzima, bila kujali gharama za kuisafirisha kufika kwa mlaji, huoni unajenga mazingira ya kuadimika kwa bidhaa hiyo? Na ni ukweli uisopingika kwamba kitu chochote kikiadimika, lazima kitauzwa au kupatikana kwa mwendo wa kuruka, hata kama utatumia polisi au makachero wangapi. Kwanza hiyo ndiyo inakuwa umewapa nafasi ya kufanya magendo na mauzo ya chini chini. Nadhani kuna umuhimu wa serikali na viongozi wa sasa kufuata msingi bora ya uchumi wa kisasa, mahitaji ya masoko huria na biashara huru, la sivyo itakuwa ni yaleyale, ya enzi za Mchonga!!!

Anonymous said...

naungana na wewe kabisa mtoa maoni, mfanya biashara alieko kando kando ya ziwa tanganyika itanufaisha vipi biashara hiyo ambayo bei ya ya dar, kigoma mjini na kirando iwe sawa, hata kama serikali itawasogezea bidhaa hiyo karibu katika miji mikubwa, lakini bado kwa mfanya biashara wa kirando anasafari kubwa mpaka aifikishe huko, je ataweza kuiuza kwa bei anayouza mtu wa mjini? hii ni ishara tosha kwa wakaazi wa maeneo kama hayo watakuwa na uadimu wa bidhaa hiyo au watainunua kwa njia ya mlango wa nyuma, kwani mfanya biashara hatoweza kutumia gharama kubwa akauza kwa bei ya chini, ataacha kuuza au atalangua. back 1947