Rais Dk.John Pombe Magufuli amelipiga marufuku shirika la ugavi wa umeme nchini Tanesco kuhakisha haliingii mkataba tena na kampuni yoyote katika kukodisha mitambo ya kufua umeme na badala yake ihakishe inajenga mitambo yake yenyewe ili kuweza kutoa huduma bora na kwa bei rahisi kwa wananchi wake.
Mh.Rais ameyasema hayo alipokuwa akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi ii jijini Dar es Salaam ambapo amesema Tanzania imechezewa cha kutosha na sasa kilichobaki ni kazit tu.
Akitoa maelezo ya mradi huo mkurugenzi mtendaji wa Tanesco Mhandisi Felchesmi Mramba amesema mradi huo utagharimu dola za kimarekani milioni 344 na utakamilka ndani ya miezi 28.
Naye balozi wa Japan hapa nchini ambao ndio wafadhili wakubwa wa mradi huo amesema ujenzi wa mtambo huo ni muendelezo wa miradi mingini na mizuri baina ya Tanzania na nchi yake.
Baadhi ya wananchi walijitokeza kushuhudia uwekwaji wa jiwe hilo wamempongeza rais Magufuli kwa hatua hiyo huku baadhi ya wananchi wakionesha shauku kubwa ya kutaka kusalimiana naye hatua ambayo iligonga mwamba kutokana na walinzi wake kuimarisha ulinzi.
1 comment:
Mheshimiwa Rais, kazi ya mikataba ya kufua umeme imekuwa gumzo kubwa Tanzania miaka na miaka. Nini kazi kubwa ya shirika la TANESCO!! Na endappo mikataba kama ya IPTL hautaendelea kama unavyodai ni wazi kwamba yote yalliyofanyika chini yake na ikiwepo uchotaji wa fedha na Iliyoitwa ESCROW ESCROW ESCROW iliyotetemesha nchi, sina ubishi kabisha na nina imani na wewe kwamba unaweza kuamuru wote waliochota hizo fedha wazirejeshe, kwani ni maajabu hata aliyesismamia swala hilo yuko huru sana na benki inaendelea kufanya mitaala ya kifedha. Hebu tumbua hilo ni jipu la hatari sana halina sababu ya kulikalia kimya. Asante.
Post a Comment