Baada ya Rais John Magufuli kuwaagiza wakuu wa mikoa wapya kuwakamata vijana wote ambao wanacheza (poolTable) nyakati za asubuhi, kwa madai kuwa wajiingize kwenye shughuli za ufanyaji kazi,
Naye,Waziri nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mtaa, George Simbachawane amemtaka mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuhakikisha anawaaondoa wapiga “debe” wote kwenye vituo vya mabasi kwa madai kuwa wanafanya vitendo vya kihalifu. Waziri Simbachawene ametoa agizo hilo jana Jijini Dar es Salaam, wakati wa semina kwa wakuu wa mikoa wote nchini ambao waliapishwa juzi na Rais Magufuli,
Ambapo alitumia nafasi hiyo kwa kusema kazi ya kupiga debe sio rasmi na aina kipato kitachoweza kumkwamua kijana kuondokana na tatizo la umasikini,
“Yaani hata hapa Dar es salaam namuomba mkuu wa mkoa ahakikishe anawondoa hawa wapiga debe kwenye vituo vya mabasi kwani wamekuwa wakichangia kutokea kwa uharifu, kipato cha mpiga debe kwa siku hakiwezi kumkwamua kimaisha sana sana wanatumia nafasi hiyo kufanya uharifu wanatakiwa kuondolewa haraka waende kwenye kazi hata za kilimo”amesema Simbachawene.
Hata Hivyo Waziri Simbachane ametumia nafasi hiyo kuwataka wakuu wa mikoa kufanya kazi kwa ufasaha na kuwatumikia wananchi ikiwemo kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi CCM.
1 comment:
Nadhani ni wakati muafaka kila mmiliki wa daladala kujiwekea utaratibu wa kupata mapato ya biashaara yake. Kwani hawa wapiga debe kwanza ni vutugu tupu, matusi maadili hawana na uvaaji wao unatianaibu taifa! Na wapiga viroba hasa hela yao kama unavyosema haina mwendelezo wowote zaidi ya viroba! Hakuna abiriabasiyejua basi lake! Isitoshe dereva na kondakta wapo sasa mpiga debe kwa sh. Mia tu wapi? Abiria tunazidiwa uoga na hasasie kina mama! Jingine wafanya biashara ya big G, maji, vyakula vya mkononi kwenye box vikomeshwe kwani vijana wadogo taifa la kesho hawasomi tunaunda taifa gani??
Post a Comment