ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, March 15, 2016

UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA KAMISHENI KUHUSU HALI YA WANAWAKE

Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake, umeingia katika siku yake ya pili kwa Wajumbe wa mkutano huu kuendelea kubadilishana uzoefu na kuelimishana kuhusu namna ambavyo kila nchi kwa nafasi yake na uwezo wake inavyotekeleza sera, sheria, na mipango inavyolenga katika kumuwezesha mwanamke kiuchumi, kijamii, kisheria na fursa mbalimbali zikiwamo za usawa wa kijinsia.
Ujumbe wa CSW 60 ukipozi katika Bendera ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa na Mwenyeji wao, Balozi Tuvako Manongi wa tatu kushoto na Afisa wa Uwakilishi wa mwisho kulia, Bi. Ellen Mahudu
Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano huu unaongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu. Katika Ujumbe yupo pia Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii, Mhe. Peter Serukamba ( Mb), Bi Mhaza Gharib Juma, Bi. Halima Omar Kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar , Bi Bengi Mazana Issa,na Bi. Constancia Gabusa

No comments: