ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 14, 2016

Utafiti: Tanzania Yabainika Kuwa Nchi ya Kwanza Isiyo Aminifu Duniani.....

Utafiti huo umebainisha kuwa uaminifu binafsi huwa mkubwa kwenye jamii zenye matatizo machache ya rushwa, ukwepaji kodi na utapeli wa kisiasa.
Wakati ambapo Austria, Uholanzi na Uingereza zimeshika nafasi ya kwanza katika nchi aminifu duniani, Tanzania na Morocco ambazo ubora wa taasisi zake ulibainika kuwa wa chini, zilifanya vibaya.


Utafiti huo ulifanywa na chuo kikuu cha Nottingham na kuhusisha nchi 159.
Walitumia taarifa zilizopo kuanzia mwaka 2003 za utapeli kisiasa, ukwepaji kodi na rushwa.

Utafiti huo ulibaini kuwa watu wanaoshi kwenye nchi zenye matukio machache ya uvunjaji sheria, walikutwa na uwezekano mdogo wa kudanganya ili kupata fedha ukilinganisha na nchi zenye matatizo ya rushwa.

Ulidai kuwa uwepo wa matukio ya uvunjaji sheria, huwafanya watu kupindisha ukweli.

7 comments:

Anonymous said...

Kumbe ni ya mwaka 2003? Mbona sijaona Kenya (Rais wa nchi hiyo alikiri mwenyewe kuwa wakenya ni waongo na hawana uaminifu) Vipi kuhusu Burundi na Somalia? Nigeria? Etc etc.

Anonymous said...

Rubbish, tuonyeshe nakala ya utafiti huo na methodology iliyotumika. Chuo cha Nottingham? Hao watafiti duni, hawana credibility hao wazungu. Hao Waingereza honest namna gani wakati wametuiiba na kupora rasilimali nyingi wakati wanatutawala barani Afrika na kuziacha nchi zetu masikini? Let them shut their mouths, sisi tupo imara na tutaendeleza nchi yetu pole pole bila handouts zao za kikoloni.

Anonymous said...

Wala sibishi wabongo sisi ni waongo kwa kila kitu kuanzia mahusiano mpaka makazini,ila wanaijeria walipaswa wawe wa kwanza wametuzidi.

Anonymous said...

Haya kazi kwa wale wasemaji wa Mambo ya Nje. Jipu lingine hilo la kutumbua. Msisubiri mpaka baada ya mwaka mmoja ndio muanze kulalamika Kama Tanzania Tourist Bodi - TTB na yule mama aliyedai Olduvai iko Kenya

Anonymous said...

Tusipingane na hii report hata kidogo. Nikiwa kama mtanzania tena wa kujivunia lakini ukweli ni kwamba sisi watanzania tuna tatizo katika suala la uaminifu tusikatae hata kidogo. Ni garbage report lakini huo ndio ukweli na ukweli siku zote hasa kwa waafrica ni wimbo unaochukiza katika masikio yetu. Kama mtanzania namuunga mkono kwa vitendo muheshimiwa raisi wangu mpendwa Magufuli katika kupambana na tabia chafu ya udanganyifu na uzembe. Hapa kwetu New York tunasema when you see something say something don't keep it to yourself. Na sisi watanzania wakati umefika tunapoona kuna vitu hatarishi kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi yetu kutokaa kimya badala yake tunatakiwa kukemea au kutoa taarifa katika taasisi husika ili kuzuia uharibifu huo.

Anonymous said...

Haitaji nakala kila kitu kilivyokuwa vinaendeshwa na tawala zilizo pita viko wazi. Viongozi sio waminifu mpka nyanja zote ziko hivyo. Ila magufuri baba ana kazi ya kusafisha. Na Mungu amuongoze

Anonymous said...

Wakoloni toka lini wakawa waaminifu???Research yangu nimeanzia miaka 300 iliyopita. Data zinaonyesha wakoloni sio tu
Wamekosa uaminifu Bali pia ni waroho waliojaa unafiki na ujambazi..tumepuuzwa kiasicha kutosha. Wapeleke utafiti wao chooni.