ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 18, 2016

Vigogo Meno ya Tembo Wahukumiwa Miaka 30 jela


Mshitakiwa wa pili,Yu Fujie (kushoto) na Huang Gin wakiwa katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wakiingizwa katika chumba cha mahakama na askari magereza.

Wakijuta baada ya kuhukumiwa.

VIGOGO wawili raia wa Kichina, Huang Gin na Yu Fujie waliokamatwa mwaka 2013 wakituhumiwa kukutwa na meno ya tembo wamehukumiwa kwendea jela miaka 30 au kulipa shilingi Bilioni 54 kila mmoja.

Raia hao wamehukumiwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam chini ya Hakimu Mkazi, Cyprian Mkeha ambapo kesi hiyo ilichukua muda wa zaidi ya saa 5 kusomwa huku upande wa serikali kupitia kwa Wakili wa Serikali ukiongozwa na Faraja Nchimbi ambaye alikuwa na mawakili wengine ambao ni Paul Kadushi,Wankyo Simon pamoja na Salim Msemo ambapo kwa upande wa washitakiwa waliwakilishwa na Wakili Nehemiah Nkoko ambaye alijaribu kutoa hoja zake ikiwemo kuiomba mahakama iwapunguzie adhabu.

Watuhumiwa wote walisomewa mashtaka matatu ambayo ni kwanza, kukamatwa na nyara za serikali ambazo ni meno ya tembo, shitaka la pili, kutumia pesa walizokutwa nazo katika upekuzi kuwashawishi maofisa wa serikali ili wawaachie na shitaka la tatu, kukutwa na ganda la risasi katika nyumba waliyokuwa wakiishi ambapo shitaka hilo la tatu lilitupiwa mbali na kubaki mawili yaliyowatia hatiani.

Akisoma vifungu vya sheria, Hakimu Mkeha alisema kuwa watuhumiwa walikamatwa Novemba 2013 katika nyumba waliyokuwa wamepanga iliyopo Mikocheni jijini Dar, wakiwa na vipande vya meno ya tembo 728 ambapo ni sawa na tembo waliouawa 226 na kusema kuwa waliisababishia serikali kupoteza fedha nyingi na kuingizwa katika kesi ya uhujumu uchumi. Pia mahakama iliamuru magari yao matatu waliyokutwa nayo kutaifishwa.

Na Denis Mtima/Gpl

2 comments:

Anonymous said...

Sasa tangu 20013 mpaka hii leo kitu gani kilichokuwa kinachelewesha hao wachina wahujumu wa uchumi kuchukuliwa hatua wakati kila kitu cha ushahidi kipo kama hawa wachina wangekuwa wamefanya upuuzi huu kwao china mbona zamani sana wameshahaulika nao wenyewe wanalijua hilo. Ndio yale aliyoyasema muheshimiwa Maghufuli kwamba mtu kakamatwa na visibitisho vyote vya uhalifu alioutenda kwanini kesi ichukuwe miaka mitatu kama si kutafuta mianya ya rushwa kitu gani? Kuna wale watu wanaojifanya wanajua wakaanza kumlaumu raisi kwa kusema muheshimiwa raisi anaingilia nguvu za mahakama? Mimi bila woga au kutafuna maneno hawa watu wanaojifanya wasomi maandazi wanaomlaumu Maghufuli kwa kauli yake ya kuziomba mahakama kuharakisha kutoa maamuzi ya haraka kwa kesi ambazo zina ushahidi wote wa muhusuka kutenda kukosa nawaita wapumbavu na hapana shaka hao ni miongini mwa watu walioifikisha Tanzania pabaya hapa ilipo. Maghufuli amethibitisha si mara moja wala si mara mbili yakwamba ni mweledi wa mambo ya kiutawala wa kiwango cha ajabu. Hivi karibuni alipoteuwa wakuu wa mikoa na kuwapa nafasi baadhi ya majenerali wa jeshi watu wale wale wanaojifanya wanajua kama kawaida hawakuacha kupanua midomo yao kupinga uteuzi huo hata bila ya kuuliza au kufanya uchunguzi kwanini muheshimiwa raisi kawachagua wale wanajeshi wawe wakuu wa mikoa? Ikumbukwe tangu day one Magufuli alipoingia ikulu au kabla hajaingia ikulu anayafahamu matatizo ya kila mkoa kwa undani zaidi ni mtu alietembea karibu Tanzania nzima wakati wa campaign kata kwa kata,tarafa kwa tarafa,kaya kwa kaya,wilaya kwa wilaya na mkoa kwa mkoa kusikiliza matatizo ya wananchi napata taabu sana nikimuona mtu anapinga au kutoa maelekezo ifanyike vile anavyohisi yeye kinyume na kile anachokifanya muheshimiwa raisi wakati mtu huyo pengine hayupo hata huko Tanzania na mbaya zaidi pengine hajakanyada Tanzania kwa miaka kadhaa sasa. Muheshimiwa Maghufuli amewateua wakuu wa mikoa wanajeshi zaidi kwa ile mikoa ya mipakani mwa nchi yetu na hii inatokana na kuwepo kwa kushamiri kwa vitendo vya kihalifu katika maeneo hayo. Kwa mfano utamlaumu vipi Uhuru kenyata kumteua mkuu wa mkoa mwanajeshi katika mkoa wa kenya waliopakana na somali? Kila mtanzania anahofia kuingizwa kwa silaha nzito kutoka nchi jirani kama vile Congo,Burundi hata Uganda zinazotumika katika vitendo vya kihalifu. Kunauwezekano kabisa kwa kudhibiti vitendo vya kihalifu katika mikoa ya mipakani ni mrubaini wa kuzuia vitendo vya kihalifu jijini daresalam kwa kuwa kule mipakani ni chanzo na makimbilio ya wahalifu. Kama watanzania twenye uchungu na nchi yetu tunatakiwa kumuunga mkono muheshimiwa raisi kwa dhati kabisa sio kwamba hatakiwi kupingwa kutokana na baadhi ya maamuzi yake hapana don't take me wrong,lakini mpaka hivi sasa nikiangalia hao wanaompinga naona ni watu wa bias zaidi kuliko facts.

Anonymous said...

Safi sana naona agizo la raisi wiki zilizopita juu ya mahakama zimeanza kufanya kazi.