Wananchi jamii ya wafugaji wakiwa wamebeba Mabango yenye ujumbe mbalimbali wakipinga hatua ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amosi Makala kurejesha ardhi ya Shamba la Lokolova kwa chama cha Ushirika wa Wakulima, wafugaji na uzalishaji mali cha Lokolova.
Msemaji wa jamii ya wafugaji Ismail Sevule (mweye kofia ya kijani) akiwa na wananchi hao wakiimba kupinga hatua hiyo.
Mifugo ilikuwa sehemu ya mkusanyiko wa kuondi hilo la wananchi katika eneo hilo ambalo mgogoro wake unatajwa kuwa ni wa zaidi ya miaka 30 sasa.
Wananchi wakiongozana na mifugo wakiimba nyimbo mbalimbali kuonesha kupingana na kauli ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ya kurejesha shamba hilo kwa ushirika.
Wananchi wakipiga Push Up wakati wa mkusanyiko huo.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
MGOGORO wa kugombea ardhi ya shamba la Lokolova lenye ukubwa wa ekari 2,470 lililopo kata ya Makuyuni wilaya ya Moshi vijijini umeibuka upya huku wananchi jamii ya wafugaji wakimbebesha lawama mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amosi hatua yake ya kutangaza kurejeshwa ardhi hiyo kwa chama cha Ushirika wa Wakulima ,wafugaji na uzalishaji mali cha Lokolova.
Mgogoro huo wa zaidi ya miaka 30 sasa ,umeibuka baada ya kundi kubwa la wananchi hao kukusanyika katika eneo hilo wakiwa na mifugo yao pamoja na mabango yenye ujumbe mbalimbali huku wakiimba kuonesha kupinga hatua hiyo ya serikali wakidai itachochea kuibuka kwa mgogoro uliokuwepo.
Februari 19 mwaka huu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Makala akiwa ameongozana na viongozi wengine kutangaza maamuzi ya kikao cha Kamati ya Ushauri ya mkoa kurejesha shamba hilo kwa Ushirika wa Lokolova hatua ambayo imefuta mpango wa awali wa serikali ulioasisiwa na mtangulizi wake (Leonidas Gama) wa kulifanya eneo hilo la ardhi litumike kujenga soko la kimataifa na mji wa viwanda.
Katika mkutano wake wa hadhara na wanachama wa chama cha ushirika cha Lokolova pamoja na wananchi wa eneo hilo Makala aliweka bayana hatua zilizofikiwa na kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC) kilichokutana Feb.12 Mwaka huu Mjini Moshi kuwa Serikali imeridhia kurudisha shamba lenye ukubwa wa ekari 2,470 kwa wanaushirika.
Kiongozi wa wananchi Jamii ya wafugaji washio vijiji vya Lotima na Makuyuni Ismail Sevule alisem katika tamko lao kuwa wanapinga hatua ya mkuu wa mkoa (Makala) kurejesha ardhi hiyo ya Shamba la Lokolova kwa chama cha Ushirika ,Ushirika ambao walida ulikwisha futwa tangu mwaka 2014.
“Tunatoa tamko la kupinga hatua ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro kurejesha ardhi ya eneo la Lokolova kwa chama cha ushirika ,wanaushirika ambao si wa kata ya Makuyuni ,watu hawa waliingia kwa mbinu katika ushirika uliokuwepo ,hata hivyo bado ushirika huu ulifutwa tarehe 1 4 ,mwezi wa tatu mwaka 2014 na kutangazwa katika gazeti la serikali la tarehe 23/5 mwaka 2014 “.alisema Sevule.
Alisema wananchi jamii ya wafugaji wamepigwa butwaa kutokana na kauli ya mkuu huyo wa mkoa huku wakieleza kutokubaliana na uamuzi huo wakitaka kujua ushirika ulifutwa kwa vigezo gani na unarudishwa kwa vigezo na utaratibu gani .
“Sisi wananchi kata ya Makuyuni tunataka kujua ushirika ulifutwa kwa v igezo gani na unarudishwa kwa vigezo gani ,mkuu wa wilaya ametangaza pia eneo limesitishwa kilimo kwamba baada ya miezi mitatu wana ushirika watakuja na Mastaer Plan yao ya kufanya kazi katika eneo hili,tunaiambia serikali hatukubalina na utaratibu huo.”alisema Sevule katika tamko lao hilo.
“Hati miliki ya eneo hili ilitolewa kinyemela mwaka ,1987,hati hiyo ilitolewa wakati huo kukikiwa na mgogoro.watu wa ardhi walifanya makosa kutoa hati wakati eneo likiwa na mgogoro ,tutaenda mahakamni kudai utolewaji wa hati hiyo si halali”aliongeza Sevule.
Alisema licha ya kuwepo kwa zuio la kufanya shughuli yoyote katika eneo hilo ikiwemo Kilimo ,wafugaji hao wameeleza kuendelea kulisha mifugo ya katika eneo lilopewa jina la Phase 2 huku wakiongejea utaratibu wa serikali juu ya matumizi katika eneo lililopewa jina la phace 1.
“Tunaomba serikali ijue hivyo na kuanzia leo eneo hili tunaendelea kuchunga eneo la phace 2 na phase 1 tunangojea utaratibu wa serikali….lakini wakiingiza hawa wanaoleta Master plan tutapambana nao “alisema Sevula.
Akielezea historia ya mgogoro huo mmoja wa wananchi hao, Hashim Mandale alisema umeanza tangu mwaka 1983 hadi sasa huku akieleza kuwa wapo baadhi ya wafanabiashara na viongozi ndio wanaasisi mgogoro huo.
“Eneo hili liko ndani ya vijiji viwili vya Lotima na Makuyuni ,tulipo zaliwa sisi,kulianzishwa Ushirika wa wafugaji ambapo walitoa ng’ombe, eneo hili likagawanywa Phace 1 na Phase na eneo la phase 1 watu wote wa Tambarare tuliridhia kulitoa kwa serikali kwa ajili ya kujenga soko la kimataifa.”alisema Mandali.
“Tunashangazwa leo hii tumekuja kuona maeneo yote mawili yanachanganywa na kuwa kitu kimoja na hawa watu wana sema ni eneo la ushirika na warudishiwe wana ushirika maana yake mkuu wa mkoa ndiye atakua ameanzisha upya mgogoro huu.”aliongeza Mandali.
Mwenyekiti wa chama cha Ushirika huo ,Samwel Lyimo alisema anavyotambua yeye hakuna mgogoro kati ya Wakulima na Wafugaji katika eneo hilo isipokuwa kuna watu ambao wamevamia eneo na kufanya shughuli za kulisha mifugo yao.
Tangu mwaka 2011 serikali mkoani Kilimanjaro ilikusudia kulitaifisha shamba hilo lenye ukubwa wa zaidi ya ekari elfu 2,470 ili kuepusha mgogoro wa ardhi baina ya wakulima na wafugaji wa maeneo ya Lotima na Makuyuni waliokuwa wakigombania shamba hilo la Lokolova kwa ajili ya Kilimo na Malisho.
No comments:
Post a Comment