Wanawake wa Mkoa wa
Dodoma wanaonufaika na Mradi wa Manjano Dream Makers wakikisikiliza kwa
Makini Mada Kuhusu Elimu ya Biashara na namna ya kuendesha Ujasiriamali
Kwenye Mafunzo Yanayoendelea Mkoani Dodoma.
Mafunzo ya kuwawezesha
wanawake kiuchumi kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano yameanza mkoani
Dododma. Jumla ya Washiriki 30 wamechaguliwa katika fursa hiyo na wanajulikana
kama Manjano Dream Makers. Mafunzo hayo yamegawanyika katika awamu mbili. Awamu
ya kwanza wanawake hao kutoka Manispaa ya Dodoma watapatiwa elimu kuhusu sifa
za ujasiriamali, changamoto zake na namna ya kukuza na kuendesha biashara ikiwa
pamoja na nidhamu ya kutunza pesa na mahesabu yaani 'Financial literacy'. Pia
washiriki watanufaika namna ya kutoa huduma nzuri na bora kwa wateja na kujua
mbinu zipi watumie kujiwekea akiba.
Awamu ya pili washiriki watapatiwa elimu kuhusu matumizi sahihi ya Vipodozi hasa "Make-Up Artistry". Awamu hii hapa washiriki watajua matumizi yenye ueledi (professional) wa kutunza ngozi, kutumia vipodozi na namna ya kuwapamba maharusi na wakazi wa Dodoma na maeneo jirani kwa kutumia vipodozi sahihi na salama. Mara baada ya mafunzo haya washiriki watapata fursa ya kukopeshwa mitaji kwa ajili ya biashara kwa lengo la kuwakwamua washiriki wote kuondokana na ukosefu wa ajira na kujikita katika kujiajiri katika tasnia ya vipodozi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shera
Illusions Africa na Mkurugenzi wa Manjano Foundation Mama Shekha Nasser
Akieleza Machache leo wakati wa Mafunzo ya Ujasirimali kwa Wanawake wa
Mkoa wa Dodoma.
Mafunzo haya yanaratibiwa na Taasisi ya Manjano Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Shear illusions kupitia vipodozi Pendwa vya LuvTouch Manjano. Mafuzo kama haya tayari yamesha wanufaisha wanawake Zaidi ya 150 Kutoka Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Visiwani Zanzibar. Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo kutoka Mkoa wa Dodoma wameishukuru Taasisi ya Manjano Foundation kwa kuwapa nafasi hiyo na kuwaletea mradi huo.
Picha ya Pamoja ya Washiriki
wa Mafunzo ya Ujasiriamali kutoka Mkoa Dododma.
Wakieleza zaidi wamesema
walikuwa na hamasa sana tangu walipopata taarifa kwa wanawake wenzao wa mikoa
ya Dar es salaam, Mwanza, Arusha na Zanzibar kunufaika na mradi huu na walikuwa
wanasubiri kwa hamu kubwa sana mafunzo hayo. Wakiendelea zaidi wamesema wapo
tayari kupigana na kujikita vizuri kupitia mradi huu kwa lengo la kujikwamua na
kujiongezea kipato kupitia kazi ya mikono yao.
No comments:
Post a Comment