Dereva na mtuhumiwa raia wa Msumbi akiwa chini ya ulinzi
Sehemu ya 'mzigo' huo
Askari polisi akichana tenki la mafuta la gari hilo
Madawa ya kulevya aina ya heroin yanayokadiriwa kuwa na thamani ya Rand za Afrika Kusinu milioni 50 yamekamatwa yakisafirishwa ndani ya tenki la mafuta la gari lililokuwa likielekea Gauteng kutokea Msumbiji.
Habari zinasema hilo limetokea baada ya kikosi cha askari polisi wa mbwa cha Whiteriver walifanikiwa kukamata madawa hayo baada ya kusimamisha gari aina ya Toyota Prado lenye kutia mashaka katika geti la kulipia ushuru wa barabara eneo la Nkomazi huko Mpumalanga siku ya Jumapili iliyopita.
Baada ya upekuzi mbwa wa polisi alipata harufu katika moja ya matenki ya gari hilo na kubweka kuwa mna 'mzigo', ndipo baada ya kufungua tenki hilo na kulichana wakakuta 'unga' huo umefichwa ndani ya tenki hilo ukiwa umefungashwa kwenye vifuko vya plastiki, alisema msemaji wa Polisi Sajini Gerald Sedive.
"Madawa ya kulevya yenye thamani ya R50 milioni yalikutwa kwenye tenki la mafuta. Gari lilikuwa likitokea Msumbiji", alisema, na kuongezea kwamba dereva wa gari hilo raia wa Msumbiji ametiwa mbaroni na hatua za kisheria zitachukua mkondo wake.
No comments:
Post a Comment