Na Mwandishi WetuBondia Abdalla Pazi 'Dula Mbabe' baada kumsambalatisha Mada Maugo kwa TKO ya raundi ya tatu mpambano uliopita uliofanyika jumapili ya pasaka katika uwanja wa ndani wa Taifa
sasa ameingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mpambano wake mwingine wa kimataifa utakaofanyika uwanja wa ndani wa Taifa siku ya mei 14
Akimkabili bondia Chamunorwa Gonorenda kutoka Zimbabwe bondia Pazi amesema kuwa yeye ni tingatinga la kuchonga barabara hivyo achagui bondia wa kucheza nae aliongeza kwa kusema kuwa vichapo vyangu vinaeleweka kuwa mabondia wote ninaokutana nao awamalizi raundi nilianza hivyo china nikampiga bondia raundi ya nne nikaja bongo nikampiga K,O mbaya sana bondia Baraka Mwakansope
Baada ya hapo nikapambana na Mada Maugo ambaye kwa sasa ataki ata kuniona na akisikia jina la Dula Mbabe anakaa kimyaaa hivyo nataka niendeleze rekodi yangu hii na sito waangusha mashabiki zangu
katika mpambano huo kutakuwa na mipambano mbalimbali ya kimataifa itawakaokutanisha na mabondia wa Tanzania na wa nchi nyingine mbalimbali
ambapo Thomas Mashali atakuwa akigombania ubingwa wa Dunia wa W.B.O akipambana na Sajjad Mehrab kutoka 'Irani'
mapambano mengine ya kimataifa yatawakuanisha bondia mwanadada Lulu Kayage na Chiedza Homakoma 'Nikita' Malawi mabondia wengine ni Ramadhan Shauri atakaepambana na Osgood Kayuni wa Malawi wakati Twaha Kassim atapambana na Fred Nyakese kutoka Kenya na Saleh Mkalekwa atakumbana na Jems Onyango wa Kenya na Fransic Miyeyusho atavaana na Frank Kiwalabye wa Uganda na Nassibu Ramadhani atacheza na Edwrd Kakembo wa Uganda
mapambano mengini ni kati ya Shaban Kaoneka atakaecheza na Hassan Mwakinyo na Issa Nampepeche atakumbana na Baina Mazola
mapambano hayo ya kimataifa yameandaliwa na promota mkongwe Ally Mwazowa kutoka mkoa wa Tanga
siku hiyo kutakuwa na burudani mbalimbali zitakazo sindikiza mapambano hayo ya kimataifa ya mchezo wa masumbwi
siku hiyo pia kutakuwa na ugawaji wa zawadi kwa mabondia watakaocheza vizuri na kuonesa nidhamu ya mchezo wa masumbwi ikiwemo vifaa vya mchezo pamoja na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutamba shiria za mchezo uho nyingine zitakuwa zikiuzwa kwa galama nafuu kwa mashabiki watakaofika siku hiyo
No comments:
Post a Comment