ANGALIA LIVE NEWS

Monday, April 11, 2016

BREAKING NEWS: RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA ANNE KILANGO MALECELA KUANZIA LEO.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzanaia Dr.John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa mkoa wa shinyanga Ana kilango Malecela kuanzia leo.
Utenguzi huo umetokana na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Ana kilango Malecela kutungaza kwenye vyombo vya habari kuwa mkoa wake hauna watumishi hewa jambo ambalo lilisababisha Ikulu kufanya uchunguzi wake na kubaini kuwepo kwa wafanyakazi hewa 45 katika awamu ya kwanza na awamu ya pili ya uchunguzi bado inaendelea.

Akiongea Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akipokea hundi ya shilingi bilioni sita zilizotolewa na Ofisi ya Bunge baada ya kubana matumizi kwa ajili ya kununulia madawati Rais Magufuli ameeleza kusikitishwa na hali hiyo na kuagiza Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala wa Mkoa kuondolewa ofisini mara moja.

2 comments:

Anonymous said...

Hii ndiyo kazi ya msema ukweli ni mpenzi wa mungu. JPM.....mama wa watu kajaribu kufunika maovu kumbe mzee kiona mbali kamuona mapema. Hizi ni zama za uwazi na ukweli. Hongera JPM na upinzani ongeza pressure wezi na walongolongo watapungua kama sio kuisha kabisa...Nimeanza kumpenda mwanawane. Yale ya Mwenzetu,brother brother hakuna.fanya kazi,lipwa mshahara wako,sema ukweli mungu atakukingia kifua.

Anonymous said...

Mama kakurupuka katika kauli yake. Alitakiwa kuwa makini kwani watengezaji wa mishahara hewa ni maofisa watumishi wa serikali waliomo ndani ya system kuwabaini kwake kunataka kiongozi makini, kwa point hii mama sio kiongozi makini anaweza kuendana na kasi ya mueshimiwa raisi ya kuisafisha Tanzania kutokana uozo wa ajabu wa watumishi wa umma..