Dkt.Kigwangalla akagua Hospitali ya Taifa ya Kifua Kikuu Kibong’oto iliyopo Mkoani Kilimanjaro
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla, ametembelea Hospitali ya Taifa ya Kifua Kikuu Kibong'oto eneo la Sanya Juu Wilani Siha Mkoani Kilimanjaro.
Dkt. Kigwangalla katika Hospitali hiyo, alipata kitembelea maeneo mbalimbali ikiwemo wodi za wagonjwa wa Kifua Kikuu (TB) ya kawaida na ile kali ambapo pia aliweza kutembelea eneo la kituo cha utafiti cha magonjwa hayo pamoja na Maabara.
Kihistoria Hospitali hiyo ya Kibong’oto ilifunguliwa rasmi 29 Oktoba mwaka 1952 na Lady Twining, baada ya miaka saba ya vita ya pili ya dunia chiniya utawala wa Muingereza na imekuwa ikitoa huduma hiyo ya magonjwa ya kuambukiza hususani Kifua Kikuu.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga amemwelezea Naibu Waziri changamoto mbalimbali ikiwemo suala la nyumba za watumishi na mambo mengine ikiwemo suala la bajeti ya vifaa tiba.Tazama MO tv, kuona tukio hilo:

Msafara huo ukirejea katika maeneo mengine wakati wa ukaguzi na Naibu Waziri wa Afya Dk.Kigwangalla.
Pichani wote waliovaa 'mask' maalum ni kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya vijidudu vya ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) hasa kwa upande huo wa wagonjwa maalum wa TB sugu.ambao wapo upande maalum. Hivyo kuvaa kifaa hicho kinasaidia kupunguza hali ya maambukizo wakati wa kufika eneo hilo kama sheria na taratibu zilizowekwa kitaalam na uongozi wa Hospitali hiyo.
No comments:
Post a Comment