Dar es Salaam. Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wa Idara ya Sayansi na Uhandisi wa Kompyuta (CoICT), Dk Richard Mgaya amefariki dunia baada ya kuteketea kwa moto akiwa ndani ya gari lake aliyokuwa akisafiria kurejea nyumbani.
Msemaji wa Jumuiya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udasa), Dk Kisaka Mussa alisema jana kuwa Dk Mgaya alifariki Jumapili wiki iliyopita asubuhi. “Taarifa tulizonazo ni kwamba alikuwa anatoka mitaa ya Africana kwenda nyumbani, akiwa njiani aligonga lori baada ya muda wakati akiendelea na safari yake, gari yake ilipata moto na kuugua,” alisema Dk Mussa.
Alisema wakati gari yake ikiteketea, Dk Mgaya hakufanikiwa kuokolewa kutokana na moto mkali, hata yeye hakuweza kutoka, hivyo aliteketea akiwa ndani.
“Tulipata taarifa zake kupitia kwenye mitandao ya jamii na baadaye kujiridhisha kupitia namba za gari aliyokuwa akiendesha,” alisema Dk Mussa.
Taarifa zilizosambazwa mitandaoni zikimkariri Mkuu wa Idara hiyo, Dk Honest Kimaro akisema kuwa kabla Dk Mgaya alipata ajali iliyosababisha gari lake kuteketea moto akiwamo ndani. “Kwa ujumla tumeshtushwa sana na msiba huu. Dk Mgaya alijiunga na idara yetu miaka minne hivi iliyopita akitokea masomoni Marekani,” inasomeka taarifa hiyo.
1 comment:
Tanzania yetu vikosi vya dharura na zima moto viko wapi? JPM zile garibza polisi kwa ajili ya chama zipunguze nunua gari na helikopta ya zima moto. Nyumba nyingi zinazoibuka jijini ukitokea moto tusishindwe kuokoa maisha na mali za wananchi. Nawasilisha.
Post a Comment