
Mamlaka ya Usimamizi wa Huduma za Nishati na Maji EWURA imetangaza kushusha bei za umeme kuanzia leo kwa watumiaji wote wa viwango tofauti.
Kushuka huko kwa bei ya umeme ni kutokana na ombi la Shirika la Umeme Tanzania TANESCO kutaka bei za umeme zipunguzwe sambamba na hilo gharama za huduma kwa baadhi ya wateja zimeondolewa.
Bei mpya kwa watumiaji wadogo ni sh.100 kwa uniti, watumiaji wa kati ni sh.292 toka 298 ya zamani.Wafanyabiashara wadogo ni sh. 195 toka sh. 200 ya hapo awali.
Bei mpya kwa wafanyabiashara wa kati ni sh.157 toka sh. 159. Wanaonunua kwa wingi (bulk) ni sh. 152 toka sh. 156 ya hapo awali
Tazama jedwali hili kuona mgawanyo wa bei mpya.

2 comments:
Shukrani Mhe Waziri na Serikali ya awamu ya Tano. Hawa EWURA wote ni jipu. Ni kweli watu wote hatunabudi kulipia umeme lakini wao walificha mapungufu yao katika kufuatilia kwa kuingeza grarama kwa watumiaji. Walikuwa maneno mengi kuliko kazi. Hili libadilike. Tu one matokeo ya kazi na uwekezaji wanaoufanya. Wapunguze majigambo ya kufanya kazo. Kupunguza bei ni sawa. Kwanza kutawezesha wengi kuwa na uwezo wa kutumia nishati hiyo na hivyo kupunguza uchafuzi wa mazingira. Lakini pili, kunaifanya nchi yetu kutumia nishati inayosukuma maendeleo shuleni, vituo vya afya na hata viwanda vidogo vidogo - yote haya TANESCO walikuwa hawayajali ama hawayaoni. Tubadilike tuhimize watu watumie nishati hii lakini pia walipe. Elimu kuhusu umuhimu wa kulipa na kufuatilia na kupambana na wazi wa nishati. Wenzetu TANESCO kwa bahati mbaya walionana rahisi kuongeza bei tu! Hawakuwa na mkakati mwingine. Majipu sana hawa. Hata Mkuu wa Shirika alikosa washauri.
Ukiachia EWURA, TANESCO yenyewe ni jipu.kutokana na corruption TANESCO wanafanya manunuzi ya vifaa vyao kwa bei za juu na kufanya gharama za uendeshaji za shirika kuwa za juu.
Post a Comment