ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 7, 2016

KID BWAY ATAMBULISHWA RASMI LAKE FM MWANZA

Baada ya Watu wengi kujiuliza maswali mengi juu ya alipo Sandu George, maarufu kwa jina la Kid Bway (Pichani), ambae kwa muda mrefu amejizolea sifa kubwa katika tasnia ya utangazaji na uandaaji wa muziki, ukweli ni kwamba amejiunga na kituo kipya cha redio Jijini Mwanza kiitwacho Lake Fm, Raha Ya Rock City.

Katika kurasa za Mitandao ya Kijamii za redio hiyo, kuna post ya kumtambulisha Kid Bway iliyokuwa ikisomeka "Wananzengo tunayo Furaha Kumtambulisha Mwananzengo Kid Bway @kidboytz ambae ni Mtangazaji na Mkuu wa Vipindi 102.5 Lake Fm Mwanza.

Raha yake ya Rock City ni Kuona Vipaji vya Wasanii wa Mwanza vinakua na Kutambulika hadi ngazi ya Kimataifa.

JE WEWE RAHA YAKO YA ROCK CITY NI NINI?

Follow ‪#‎LakeFm Instagram, Twitter & Facebook @lakefmmwanza

‪#‎RahaYaRockCity ‪#‎RadioYaWananzengo".

No comments: