Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (aliyevaa koti) akicheza ngoma ya asili na wananchi wa Kata ya Sumbugu wilayani Misungwi mara baada ya kuwasili katika eneo hilo kwa ajili ya kufungua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi hao. Waziri Kitwanga amemaliza ziara jimboni kwake leo na kuwaonya madaktari na wauguzi wilayani humo kuacha tabia ya kuwaomba rushwa wananchi. Picha na Felix Mwagara.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akizungumza na wananchi wa Kata ya Sumbugu wilayani Misungwi. Katika hotuba yake, Kitwanga aliwataka wananchi wa jimbo lake washirikiane ili kuliletea maendeleo jimbo hilo na kuwaonya madaktari na wauguzi wilayani humo kuacha tabia ya kuwaomba rushwa wananchi. Kitwanga amemaliza ziara jimboni kwake leo
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (katikati meza kuu) akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ihelele wilayani Misungwi. Katika hotuba yake, Kitwanga aliwataka wananchi wa jimbo lake washirikiane ili kuliletea maendeleo jimbo hilo na aliwaonya madaktari na wauguzi wilayani humo kuacha tabia ya kuwaomba rushwa wananchi. Kitwanga amemaliza ziara jimboni kwake
No comments:
Post a Comment