Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akifungua kongamano la kujadili Fursa za Uwekezaji kati ya Tanzania na Urusi lililofanyika jana jijini Dar es salaam ambalo limewakutanisha wafanyabiashara mbalimbali wa Mataifa hayo mawili.
Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akifafanua kwa waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu faida za ushirikiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Urusi utakaochangia maendeleo katika sekta za Kilimo, Usafirishaji na Nishati hapa nchini.
Waziri wa Viwanda na Biashara wa Urusi Mhe. Denis Manturov akizungumza kwenye kongamano la kujadili fursa za Uwekezaji kati ya Tanzania na Urusi lililofanyika jana Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya washiriki wa kongamano la kujadili fursa za Uwekezaji kati ya Tanzania na urusi wakifuatilia mada wakati wa kongamano hilo jana Jijini Dar es salaam.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi (kushoto) akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania Bw. Reginald Mengi jana Jijini Dar es salaam mara baada ya kufungua kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Urusi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi (wanne kutoka kushoto) akiwa na Wawakilishi wa Serikali ya Urusi, anayefuata ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Charles Mwijage akifuatiwa na Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Amina Salum Ali.Picha zote na (Fatma Salum- MAELEZO)
2 comments:
Haya ni mabaki ya "COLD WAR" tuu. Sasa MRUSI anakuja kuziba pengo lililoachwa wazi na MMAREKANI baada ya kuzitoa zile dola zaidi ya Million 400 za millenium fund? Jamani, tukumbuke kuwa uchumi wa Urusi unaanguka vibaya sana, baada ya kuwekewa vikwazo na EEU na USA. Naona Warusi wanataka kutuibia malighafi zetu tuu. Nakumbuka miaka ya 70s walituharibia sana katika migodi ya makaa ya mawe kule mkoani Mbeya. Ni muhimu nchi yetu itambue nani ni rafiki wa kweli, ingawa najua Watanzania wengi wamesoma kule Urusi enzi za socialism/Communism. Putin ni kiongozi hatari sana, nadhani dunia nzima inatambua hili, hivyo nchi yetu sharti ifungue macho.
Putin kiongozi hatari kuliko George Bush au Obama? Nani alieisambaratisha Libya,Iraq,Afghanistan,Egypt, au Arabia zima? Tuache kuwadanganya watanzania kutokana na propaganda zisizokuwa na ukweli wowote. Urusi hajaasirika na hivyo vikwazo vinavyodaiwa kumuathiri. Hao waliomuekea vikwazo urusi ndio wapo taabani. Urusi au rusia ndio kwanza anavurumisha makombora ya gharama angani. Kumbuka hata wanaanga wa kimarekani wanategemea usafiri wa urusi kwenda angani katika kituo cha kimataifa kilichopo huko. Mrusi ni mshirika wa kweli kwa nchi yeyote inayotafuta ushirikiano wa kuheshimiana bila ya kuingiliana mambo ya ndani.Kama kulikuwa na matatizo kwa wawekezaji wa kirusi Tanzania hapo mwanzo hakika itakuwa matatizo yetu sisi watanzania na ndio maana hata baada kuondoka hao warusi tumedhidi kufulia katika umasikini. Marekani ni moja ya mataifa hatari sana kuyategemea kimaendeleo. Chini ya uongozi wa Magufuli mrusi anaweza kuwa msaada mkubwa kwa maendeleo ya Tanzania.
Post a Comment