Advertisements

Saturday, April 30, 2016

KUSANYIKO LA KUMUENZI MAREHEMU ANDREW NICKY SANGA KUFANYIKA KESHO 30.04.2016, TRIPLE 7 KAWE

Ndugu zetu pamoja na Marafiki zetu, wakati huu tukiendelea kuomboleza msiba wa mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga, tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa ushiriki wenu wa hali na mali katika kuandaa safari yake ya mwisho.


Katika kumuenzi na kukumbuka urafiki wake wa kipekee, Kamati ya Maandalizi ya Dar es Salaam inawaalika na kuwakaribisha katika kusanyiko la kumuenzi jioni ya tarehe 30 April 2016 kuanzia saa 11 jioni pale Triple 7 (@777). Kusanyiko hili ni mahsusi kwa mambo mawili makubwa, moja likiwa ni kukumbuka na kuenzi maisha yake katikati yetu na pili kupashana habari za kuhitimisha maandalizi ya Safari ya kumuweka katika nyumba yake ya Milele.

Naomba tujumuike wote na tunaamini hata huko aliko atafurahi tunapomkumbuka.


Bwana ametoa na Bwana Ametwaa Jina la Bwana Lihimidiwe 

Imetolewa na Dr. George Longopa

KNY Kamati ya Maandalizi ya Dar Es Salaam
Simu 0754 870969

2 comments:

Anonymous said...

kweli inaonyesha ni namna gani alikuwa ni mtu wa watu,mi nilijua ni US kumbe mpaka nyumbani TZ wanamuandalia...hata hao wanaokaa nakusambaza kwenye mitandao maneno yakumchafua marehemu kwamba alikuwa hivi na vile wewe ni msafi vipi unayemuhukumu mwenzako ,nadhani sasa aibu zenu jinsi watu walivyo hawajayaona hayo mnayoyaongea kijana mdogo mazishi yake utadhani alikuwa kiongozi fulani wa nchi kisa roho yake ilivyokuwa nzuri kwa wenzake yaani kwa ujumla ni mtu wa watu...R.I.P KING ANDREW

Anonymous said...

He was a true definition of a full of life. May your soul rest in peace Friend. You are truly missed.