Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela Alishiriki katika kufunga mafunzo ya PUBLIC PRIVATE DIALOGUE (PPD) pamoja na kugawa vyeti. Mafunzo hayo yenye lengo la kuhimiza mijadala na mazungumzo kati ya sekta binafsi na serikali yaleindeshwa na Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam- Shule ya Boiashara (UDBS) na kudhaminiwa na mradi wa BEST-PPD. Katika hotuba yake ya ufungaji Kasesela alisisitiza sana suala la nidhamu ndio msingi wa kujenga sekta binafsi iliyo imara. Pia aliwaasa kupunguza utitili wa jumuiya za sekta bianfsini muhimu zikaungana na kujenga moja yenye nguvu. Aliwashauri halmashauri zote kufungua dawati kwa ajili ya mijadala na sekta binafsi. " Bila sekta binafsi imara uchumi wa nchi hauwezi kukua, ni muhimu sekta binafsi ikaanza kuchukua nafasi stahiki ikiwemo kutekeleza majukumu mengine kwa niaba ya serikali mfano ukuaji wa michezo mabayo inahitaji uwekezaji ili serikali iondokane na kuwekeza, nchi kama Marekani hazina wizara ya michezo" alisema. Mafunzo hayo yaliudhuriwa na wilaya za Njombe, Kilolo, Mfundi na Iringa.
No comments:
Post a Comment