Wiki iliyopita Mhe. Wilson M. Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Washington, DC, alimkaribisha Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya M. Kikwete nyumbani kwake kwa chakula cha jioni na kujumuika pamoja na ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambao walikuwa nchini Marekani kwa ajili ya kuhudhuria mikutano ya Benki ya Dunia (World Bank Group) na International Monetary Fund (IMF) tarehe 12 - 17 Aprili 2016. Kwenye ziara yake jijini Washington, Mhe. Rais Mstaafu Kikwete alishiriki katika Kongamano la Kimataifa la Afya (World Health Congress) na Mkutano wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Kushauri Namna Bora ya Kugharamia Fursa ya Elimu kwa Wote Duniani (International Commission on Financing Global Education Opportunity).
Mhe. Rais Mstaafu Dkt. Jakaya M. Kikwete akiwa na Mama Salma Kikwete katika picha ya pamoja na wenyeji wao, Mhe. Balozi Wilson Masilingi na Mama Marystella Masilingi
Mhe. Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya M. Kikwete akibadiliashana mawazo na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dr. Servacius Likwelile (kushoto), Mhe. Balozi Wilson Masilingi na Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu nyumbani kwa Mhe. Balozi , Tanzania House Bethesda, MD.
5 comments:
wabongo kukiss A....sasa mbona hamkusema wakati alivyokuja au mnaona watu watafaidi...basi mipicha yenu kaeni nayo
Huyu jamaa si ameretire, he seems to be all over the world everyweek? who actually pays for his trips?
Sijaona mtu anapenda kusafiri kama JK, last time I read he was in China
Akifanyakazi ya Umoja wa Mataifa, analipiwa na Umoja wa Mataifa. Safari ya China alilipiwa na Chama cha Siasa cha China. Hilo halina utata; lenyeutata ni nani anamlipia mkewe?
Huyu baba anapenda safari balaa mhh
Post a Comment