ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 5, 2016

MTINDO WA VAZI LA MIDABWADA'S STYLE INAZIDI KUWATIA WAZIMU VIJANA

Habari na Zainab Ally Khamis,

Uvaaji wa nguo zilizochanwa chanwa au kuwekwa vilaka kwa makusudi unaojulikana kwa jina la "Midabwada's Style" unazidi kuwatia wazimu vijana

hususan vijana wa kisasa aka Dotcom Generation hawaoni wala kusikia mbele ya vazi la midabwada, mtindo wa vazi hilo sio kitu kimya bali katika historia inaonyesha katikati ya miaka 1960s hadi mwishoni mwa miaka 1970s jamii ya vijana wa enzi hizo katika nchi z ulaya ya magharibi na Amerika haswa vijana wa kizungu walianzisha harakati na kujiita Hippie au

Hippy Movement ambao wengi wa vijana hao walitoka katika familia na wazazi matajiri mno lakini vijana hao wakawa na mavazi yenye kuchanika ,vilaka vilaka na pengine kutembea bila ya kuvaa viatu ili mradi waonyeshe

kuwa wapo katika hali duni au sawa na masikini.Lakini katika enzi hizo pia kulikuwa na harakati za vijana watanashati wenye kujipenda na kupenda utanashati wengi wao walikuwa miongoni mwa wamerekani weusi au wenye asili ya afrika hao mpaka mitindo yao ya nywele ni Afro do.

Katika miaka hii kuwepo kwa midabwada's Style ni kurudia mitindo hile hile

sema kinachozidi ni zile mbwe mbwe na Swagaz ..lazima ujue jinsi ya kudundika Midabwada's Style..tena vazi hili lina bei ya juu sana sana huko ulaya Jeans moja ya Midabwada's inafikia mpaka Euro 120= sawa na Tsh.240,00= usichangae mzazi kumununulia mwanao jeans mpya kesho ukaikuta Midabwada's,hapa bongo mtindo huu unasemekana ulianzishwa na mgonjwa wa akili chizi kejeli ambaye ni marehemu...hakuna uhakika.

No comments: