Mwanamuziki Ndanda Kosovo amefariki leo asubuhi Jumamosi April 9, 2016 katika hospitali ya taifa Muhimbili. Habari za kifo chake zimethibitishwa na King Dodoo ambaye ni mmoja ya viongozi wa wanamuziki kutoka Congo.
Katika taarifa yake alisema, Ndanda Kosovo juzi alifikishwa katika hospitali ya Mwananyamala kwa maradhi ya tumbo, Baadae hali yake iliendelea kuwa mbaya na siku ya Ijumaa alihamishiwa katika hospitali ya Muhimbili na baadae kukutwa na mauti leo asubuhi.
Ndanda Kosovo ni mwanamuziki toka Congo aliyewahi kutamba miaka ya 2000 na bendi ya wajelajela Original. Ndanda Kosovo leo ni zamu yako kutangulia, upumzike kwa amani.
Chini ni moja ya nyimbo alizotamba nazo Ndanda Kosovo enzi ya uhai wake wimbo unaitwa chini ya ulinzi.

No comments:
Post a Comment