Advertisements

Sunday, April 24, 2016

Niseme tu ya Moyoni, Hakuna tabu kama kuwa kiongozi wa nchi kama Tanzania

Tunaweza kuwa tunawaponda hawa vijana ambao ni viongozi kama vile P Makonda, Antony Mtaka, Kasesera, Polepole na wengineo lakini tusizisahau tabia zetu za asili

Kwanza nchi hii watu wake ni wanafki na vigeu geu mno wawe wanasiasa ama wananchi, wote ni vigeu geu na wafuata mkumbo tu sijui niseme bendera fuata upepo lakini sio vyema

Pili kuwaongoza wananchi ambao wanajifanya wanajua kila kitu na kwamba wanaweza kumake analysis kwa kila jambo ni hatari sana, utamkuta msukuma mkokoteni anakusimulia mambo ya ajabu kweli kumbe anajua kinyume chake na hajajua kwamba hajui na hataki kueleweshwa

Kuongoza watu walalamikaji vijana wanaochagua ajira wote wawe maofisi makubwa makubwa na wakiwa mitaani wanalalamika tu hawataki kazi ngumu wala za kipato kidogo wao bora wakae majumbani mwao

Kuongoza watu ambao wapo Radhi kudanganywa wazi wazi kwa kuwa tu anayewadanganya ni mwanasiasa wampendae

Kuongoza watu ambao ni rahisi kujilipua kisa vyama vya siasa lakini asitoe taarifa ya mvamizi haramu anayeishi mtaani kwake

Hii nchi discipline yetu ni ndogo mno, Kubebana kupo juu sana, Uzalendo bado bado, Uwajibikaji sasaiv kidogo upo boosted lakini Hatari inayotukabili siku hizi maswali ya kitaalamu yanajibiwa kisiasa

Mimi kama mwl nimewahi kuuliza ni kivipi mtoto asiyejua kusoma wala kuandika aliyejiunga na kidato cha kwanza anaweza kufaulu mtihani wa kidato cha pili?
Nikajibiwa tena na wakaguzi wa kanda kuwa wafundishwe KKK nikakaa chini nikakumbuka masomo yale ya CT (Curriculum of Teaching) na PSYCHOLOGY niliyosoma chuo sijawahi ona applicability ya hii KKK ktk shule za secondary...

Niishie tu hapo
A.J.SWAI

4 comments:

Anonymous said...

Hahahaaaa wewe mdau uliye andika hii issue una akili sanaaaa!!!ni ukwelii mtupuuu ila umesahau ya kwamba wapumbavu pia ni wengi sanaaaa halafu ni wajuwajiii na pia ni rahisi kwao kudanganywa!!!!ni vichwa maji walio wengi hasa unafiki sasaaa!!!����������������������ubarikiwe umeona mbali mdau..

Unknown said...

Sasa huyu mwalimu mbona anadhani sote tumesomea ualimu?

KKK ndio nini? Au sisi tusioijua sio walengwa?

Anonymous said...

Good analysis.

Anonymous said...

Usigombee urais Tanzania