Kwanza nchi hii watu wake ni wanafki na vigeu geu mno wawe wanasiasa ama wananchi, wote ni vigeu geu na wafuata mkumbo tu sijui niseme bendera fuata upepo lakini sio vyema
Pili kuwaongoza wananchi ambao wanajifanya wanajua kila kitu na kwamba wanaweza kumake analysis kwa kila jambo ni hatari sana, utamkuta msukuma mkokoteni anakusimulia mambo ya ajabu kweli kumbe anajua kinyume chake na hajajua kwamba hajui na hataki kueleweshwa
Kuongoza watu walalamikaji vijana wanaochagua ajira wote wawe maofisi makubwa makubwa na wakiwa mitaani wanalalamika tu hawataki kazi ngumu wala za kipato kidogo wao bora wakae majumbani mwao
Kuongoza watu ambao wapo Radhi kudanganywa wazi wazi kwa kuwa tu anayewadanganya ni mwanasiasa wampendae
Kuongoza watu ambao ni rahisi kujilipua kisa vyama vya siasa lakini asitoe taarifa ya mvamizi haramu anayeishi mtaani kwake
Hii nchi discipline yetu ni ndogo mno, Kubebana kupo juu sana, Uzalendo bado bado, Uwajibikaji sasaiv kidogo upo boosted lakini Hatari inayotukabili siku hizi maswali ya kitaalamu yanajibiwa kisiasa
Mimi kama mwl nimewahi kuuliza ni kivipi mtoto asiyejua kusoma wala kuandika aliyejiunga na kidato cha kwanza anaweza kufaulu mtihani wa kidato cha pili?
Nikajibiwa tena na wakaguzi wa kanda kuwa wafundishwe KKK nikakaa chini nikakumbuka masomo yale ya CT (Curriculum of Teaching) na PSYCHOLOGY niliyosoma chuo sijawahi ona applicability ya hii KKK ktk shule za secondary...
Niishie tu hapo
A.J.SWAI
4 comments:
Hahahaaaa wewe mdau uliye andika hii issue una akili sanaaaa!!!ni ukwelii mtupuuu ila umesahau ya kwamba wapumbavu pia ni wengi sanaaaa halafu ni wajuwajiii na pia ni rahisi kwao kudanganywa!!!!ni vichwa maji walio wengi hasa unafiki sasaaa!!!����������������������ubarikiwe umeona mbali mdau..
Sasa huyu mwalimu mbona anadhani sote tumesomea ualimu?
KKK ndio nini? Au sisi tusioijua sio walengwa?
Good analysis.
Usigombee urais Tanzania
Post a Comment