Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema wamewakamata ombaomba 45 na kuwapeleka 17 gerezani.
Akizungumza leo na waandishi wa habari Sirro amesema jeshi hilo kwa kushirikiana na ustawi wa jamii wanafanya utaratibu wa kuhakikisha watu hao wanarudishwa mikoani kwao badala ya kuendelea kuombaomba.
“Zoezi limeenda vizuri na wachache wamebakia ambao wakiwaona askari wanakimbia,” alisema Sirro.
Katika tukio jingine Jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa 96 wenye umri wa miaka 15-18 wanaodaiwa kujihusisha na matukio ya kuvamia nyumba na kuiba nyakati za usiku jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment