ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 7, 2016

SAMIA AFUNGUA KONGAMANO LA 21 KWA WATAFITI WA UCHUMI NA VIWANDA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti inayohusiana na maendeleo ya Ustawi Nchini (REPOA) Professa Yadon M Kohi, kabla ya kufungua Warsha ya 21 ya Mwaka kwa Wasomi na Watafiti wa mambo ya maendeleo ya Uchumi wa Viwanda iliyoanza katika Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Warsha ya 21 ya Mwaka kwa Wasomi na Watafiti wa mambo ya maendeleo ya Uchumi wa Viwanda iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti inayohusiana na maendeleo ya Ustawi Nchini (REPOA) Warsha hiyo imefunguliwa  katika Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki, Wasomi na Watafiti wa mambo ya maendeleo ya Uchumi wa Viwanda baada ya kufungua Warsha ya 21 ya Mwaka kwa washiriki hao inayojadili kuhusu uendelezaji wa Utafiti wa Uchumi wa Viwanda Nchini. Warsha hiyo imefunguliwa katika Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti inayohusiana na maendeleo ya Ustawi Nchini (REPOA) Professa Yadon M Kohi, baada ya kufungua Warsha ya 21 ya Mwaka kwa Wasomi na Watafiti wa mambo ya maendeleo ya Uchumi wa Viwanda  April 06,2016 katika Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar es salaam. (Picha na OMR)

No comments: