ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 27, 2016

SERIKALI YAKIRI UPUNGUFU WA SUKARI, YAAGIZA NJE YA NCHI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza maofisa biashara wa wilaya, mikoa na Taifa kukagua maghala yote ya wafanyabiashara walioficha sukari na kuwachukulia hatua.

Waziri Majaliwa alisema hayo leo asubuhi wakati akihitimisha mjadala wa hotuba ya mapato na matumizi ya ofisi yake na kuliomba Bunge likubali kupitisha.

Waziri Mkuu alisema ni kweli kwamba kuna upungufu wa sukari nchini, ingawa pia upo udanganyifu kwa baadhi ya wafanyabiashara.

Alisema takwimu kutoka kwa wataalamu zinaeleza kwamba mpaka sasa kuna tani 37,000 za sukari katika maghala nchini, lakini imekuwa haionekani kwa sababu wafanyabiashara wakubwa wameificha ili waiuze kwa bei kubwa.

“Ninawaagiza maafisa wa biashara kushughulikia suala hili, na kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika kuwa wamekwenda kinyume na taratibu  tulizojiwekea,”  alisema Majaliwa.

6 comments:

Anonymous said...

uzalendo?sasa kwanini serikali inaagiza tena sukari ya nje,kwanini msife na tai zenu shingoni?

hii ndo Tanzania.serikali ya mizuka

Anonymous said...

Taarifa ya kusena kuna upungufu wa sukari nchini Ina walakini: Msimu wa kuzalisha sukari unanza mwezi wa tano (May) katika kiwanda cha Kilombero, kiwanda cha Kagera uzalishaji utanza wa sita(June) sasa huu ulazima wa kuagiza Sukari kutoka nje unaweza kuwa justfied kivipi!!!

Badala ya kulinda viwanda vyetu vya sukari, ajira na wakulima wadogo wa miwa sisi tunakazania kufurahisha na kulinda wafanya biashara ambao hawana hata mpango wa kuungana na kujenga walao kiwanda kimoja cha Sukari nchini - wazo hilo hawana kabisa wanacho jali ni kupata hyper-prorofit na kukatisha tamaa wawekezaji.

Anonymous said...

Tatizo la serikali wanakurupuk bila ya kufanya utafiti ukweli sukari inayozalishwa ni ndogo kuliko inayotumiwa na watu so lazma waagize tu na wamuombe radhi mbunge mary nagu kwan walihic kapewa mlungura na wafanya biashara

Anonymous said...

Tuna tatizo kubwa kama nchi.Serekali yeyote inayofanya kazi kwa kutaka sifa na viongozi wake kutaka sifa za kuonekana kwenye Tv moja ya sifa yake kuu ni kulamba matapishi.Serekali viongozi wake wanapishana kwenye vituo vya TV na kuambatana na msururu wa waandishi wa habari kama wanaenda kwenye ufunguzi wa miradi ya maendeleo usitegemee ikawa na ufanisi hata kidogo.Kweli una wataalamu kibao wa mambo ya masoko hata kwa akili ya darasa la saba lazima uwaulize je uzalishaji wa viwanda vyetu vya ndani una kidhi mahitaji yetu, ukipata jibu ndio unakuja na tamko. Eti wafanyabiashara wanatuhujumu yaani kauli za kitoto kabisa, kwanini wakuhujumu kwenye sukari tu na sio bidhaa nyingine.

Walituaminisha eti kuna sukari nyingi, wakaanza kuwaandama baadhi ya wabunge ,mary nagu, Zito kabwe, Kangi Lugola, mchungaji msigwa et wanaihujum serikali kumbe wanajihujum. Siasa kwenye ukweli haina nafasi . leo watawaambiaje hao wabunge ?

aibu imewashika sasa kujifanya kujua kila kitu,wanaanza kuumbuka kimoja kimoja.Unashindwa kujitosheleza hata sukari halaf unadanganya watu kuwa tuna uwezo wa kujitegemea hatuhitaji wahisani.Ngoma ndo kwanza imeanza,mtakanusha yote..nasikia mmekwisha kanusha kuwa hamkuwaahidi laptop waalimu nchi nzima.Bado tunawasubiri mkanushe kuwa hamkuahidi milioni 50 kila kijiji. na elimu bure pia linawashindwa.AIBU IMEWASHIKA

Hii serekeli ya awamu ya tano infaa iende kwenye jumba la makumbusho kama sio la sanaaa.

Anonymous said...

Kutumbua vichunusi vya ukurutu hadharani, na kuviacha majipu yalio kuwa sugu kama tezi. kumeza matapishi kimya kimya. Ndio maana walisema bunge lisionyeshwe live, maana watumbuaji wanaaibika sasa kwa kukurupuka.

Tanzania yangu wee.agiza sukari nje tuu.

Anonymous said...

nilijua utabania kutokuiweka comment yangu sasa kama hutaki watu wa comment si uzibe sehemu ya comment.

nawe ni jipu tu unahitaji kutumbuliwa.tena jipu wewe tezi dume.