ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 7, 2016

Tumechukua hatua dhidi ya askari walinda amani: Tanzania


” Balozi Tuvako Manongi, mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa. (Picha:UN/Idhaa ya Kiswahili/Joseph Msami)

“Tumechukua hatua kadhaa, taifa limedhalilishwa” ni sehemu ya maneno ya mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini New York balozi Tuvako Manongi akizungumzia tuhuma za unyanyasaji wa kingono zinazowakabili walinda amani 11wa nchi hiyo walioko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.

Katika mahojiano maalum na Joseph Msami, balozi Manongi amesema kuwa amearifiwa na wizara ya mambo ya nje kuhusu namna tuhuma hizo zilivyokera taifa na akasema vitendo hivyo havitafumbiwa macho.

Bila kuuma maneno Balozi Manongi anaanza kwa kusema hatua stahiki zilizochukuliwa.
KUSIKILIZA BOFYA HAPA

1 comment:

Anonymous said...

kwanini tunawatetea askari waliofanya makosa?