ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 20, 2016

UFAFANUZI JUU YA GOFUNDME AKAUNTI KWA JINA LA ANDREW SANGA*

Ndugu Wanajumuiya ,

Kuna akaunti ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia gharama za matibabu ya ndugu yetu Andrew Sanga ambayo imefunguliwa na rafiki wa Andrew anayejulikana kwa jina la Julius Shayo anayeishi Morrisville, North Carolina. Akaunti hiyo ina kichwa cha habari "Drew this Is How Much We Love You" https://dm2.gofund.me/pdzvn2hw. Familia ya Andrew haina uhusiano wowote na akaunti hii . Familia inaamini itakapofika muda wa kuhitaji msaada kwa ajili ya Andrew itafuata njia sahihi za kuwasiliana na jumuiya na marafiki wote wa mgonjwa.

Mchango wowote utakaotolewa kwenye akaunti hii uwe ni kwa mapendekezo binafsi ya mtoaji.

Ahsanteni sana

Cassius Pambamaji
Msemaji THC


Ninataarifa ya muhimu sana, kutoka Wapendwa wana jumuia ya Dallas na Houston. Tunapenda kuwakaribisheni kwenye maombi ya kumwombea mwanajumuia mwenzetu Andrew Sanga abaye alipigwa risasi na hali yake siyo nzuri. Pamoja na kuwa madaktari hawana cha kufanya, Mungu wetu ni Mungu asiyeshindwa. Tafadhali ukipata message hii watumie watu wengine, ndugu, jamaa, marafiki na jumuia nyingine za watanzania na wote kutoka Africa Mashariki. Maombi ni saa moja kamili (7:00 PM USCST au 8 PM USEST).  Tafadhali, jiunge pamoja nasi kwenye maombi kwa kupiga simu  namba 218-339-8459 ikifuatiwa na Pass code 256445#.
Mbarikiwe sana kwa wale wote mlioshiriki ktk maombi ya jana usiku.
AmbapoTunamshukuru Mwenyezi Mungu amewezesha watu ***349****kushiriki pamoja kwenye Prayer Line iliyoendeshwa na UMOJA International Outreach Church of Dallas 7:00pm CT April 18, 2016 na kuambatana na maombi maalum ya kumuombea ndugu yetu ANDREW SANGA wa Houston TX ambaye yuko ICU, kutokana na majeraha ya risasi.

***UONGOZI wa Kanisa umetangaza kwamba Jumanne April 19, 2016 kutakuwa na MFUNGO maalum kwa ajili ya maisha na afya ya Mr. Sanga.
MFUNGO utakuwa 6:00am CT - 6:00pm CT

Ikimpendeza Mungu tukutane Tena kwenye Prayer Line ya 6:00am CT Kesho (April 19th).

To join please dial 218-339-8459;256445#

TAFADHALI FWD ujumbe huu kwa wengine ili tujumuike pamoja kwenye maombi.

ASANTE na Mungu awabariki🙏

UMOJA Prayer Line
Managers

******Zifuatazo ni RATIBA zetu za huduma***

PRAYER Line 218-339-8459;256445#

6:00am- 6:30am (Mon - Sat)
1:00pm - 1:30pm (Mon - Fri)
7:00pm - 7:30pm (Mon -Wed, AND Fri)

BIBLE STUDY Line (218-895-9191;123456# )
KILA Alhamisi 7:00 pm - 8:00 pm CT.

No comments: