Kuondoka madarakani kwa Mwenyekiti wa Chama cha ADC, Said Miraji Abdullah, kumetoa nafasi kwa Hamad Rashid kurithi kiti chake.
Miraji ameondoka kutokana na kutofautiana na viongozi kuhusu uamuzi wa chama hicho kushiriki uchaguzi wa marudio wa Zanzibar uliofanyika Machi 20, mwaka huu.
Chama hicho pia kimemchagua Doyo Hassan Doyo kuwa Katibu Mkuu aliyechukua nafasi ya Lydia Bendera ambaye alikuwa akimuunga mkono Abdullah kwa kutotaka chama hicho kisishiriki uchaguzi huo.
Akizungumzia hatua hiyo, makamu mwenyekiti wa ADC, Adelastella Mkilindi amesema chama hicho kimefikia uamuzi huo ili kutimiza matakwa ya kikatiba yanayotaka kuwa na uongozi kamili.
No comments:
Post a Comment