Advertisements

Tuesday, May 24, 2016

ALIKIBA AMUOMBEA KURA MSANII DIAMOND PLATNUM

Msanii Alikiba amefunguka na kusema kuwa mafanikio aliyopata toka amerudi kwenye muziki tena ndani ya muda mfupi ni sawa na kuchana msamba kwa maana siyo hatua za kawaida.

Alikiba alisema hayo kwenye kipindi cha Planet bongo ambacho kinarushwa na kituo cha East Africa Radio na kusisitiza kuwa yeye kusaini mkataba na kampuni ya ‘Sony Music’ ni jambo kubwa sana katika maisha yake ya muziki.

“Kiukweli toka nimerudi rasmi kwenye game na kutoa wimbo wa Mwana mashabiki waliupokea vizuri sana Africa Mashariki, na kadili nilivyokuja kutoa wimbo mwingine wa Chekecha walizidi kuongezeka na kujiona nina mashabiki wengi, hivyo kuja kusaini mkataba na ‘Sony Music’ ndani ya muda mfupi kwangu mimi najiona ni kama nimepiga msamba maana siyo hatua za kawaida” alisema Alikiba.

Mbali na hilo Alikiba alimuombea msanii Diamond Platnum kwa watanzania ili wampigie kura kwenye tuzo anazoshiriki sasa na kusema kuwa yeye ndiye msanii pekee anayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano hayo hivyo watanzania wampigie kura ili aweze kushinda.

Chanzo: Eatv.tv

No comments: