Advertisements

Tuesday, May 24, 2016

Kesi ya Jerry Silaa kuunguruma leo

By Hadija Jumanne, Mwananchi hjumanne@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, leo, inatarajia kutoa uamuzi wa kupokea au kutopokea kiapo cha ushahidi katika kesi ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge wa Ukonga, Jerry Silaa (CCM) dhidi ya mbunge Mwita Waitara (Chadema).
Kesi hiyo namba 10 ya mwaka 2015 aliifungua Novemba, mwaka jana dhidi ya mbunge huyo, msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Ukonga na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), akipinga ushindi wa mbunge huyo.
Wakili Mkuu wa Serikali, Gabriel Malata aliiomba Mahakama kutopokea hati ya kiapo hicho kilichowasilishwa na Silaa akiongozwa na wakili wake, Dk Masumbuko Lamwai kutokana na kukosewa.
Wakili Malata akishirikiana na Dk Onesmo Kyauke waliweka pingamizi hilo kwa kuwa kiapo hicho kimekiuka matakwa ya sheria kwa kuwasilisha nakala halisi zote badala ya nakala iliyotokana na nakala halisi.
Jana, Mahakama ilipanga kuanza kusikiliza kesi hiyo na Silaa alitarajiwa kutoa ushahidi wake mbele ya Jaji Fatuma Masengi.

No comments: