ANGALIA LIVE NEWS

Friday, May 20, 2016

GARDNER AMJIBU LADY JAY DEE, AGOMA KUOMBA RADHI

Hatimaye mtangazaji wa Clouds Fm, Gardner G. Habash amemjibu aliyekuwa mkewe, Lady Jay Dee, aliyemtaka aombe radhi ndani ya siku saba kwa kauli aliyoitoa iliyodaiwa kuwa imelenga kumdhalilisha. Katika majibu yake amekana madai hayo.

Siku chache zilizopita, Gardner alionekana katika kipande cha Video akisherehesha tukio la kumsaka mrimbwende wa chuo cha Tanzania Institute of Accountancy (TIA) jijini Dar es Salaam, ambapo alisema kuwa “yule binti sina tatizo naye, nimeshamkojoza kwa miaka kama 15 hivi…”, kisha wimbo wa ‘Ndindindi’ wa Jay Dee ukachezwa na DJ.

Kama ilivyokuwa kwa Lady Jay Dee aliyetoa siku saba za kuombwa radhi kupitia kwa mwanasheria wake Amani Tenga, Gardner amejibu kupitia mwanasheria wake Stephen Axwesso.
Katika barua yake kwa mwanasheria wa Lady Jay Dee, mwanasheria huyo wa Gardner amekiri kuwa ni kweli mteja wake alizungumza maneno hayo alipokuwa katika shughuli iliyotajwa, lakini alidai kuwa hakuna sehemu aliyomtaja mkewe huyo wa zamani.

Alisema kuwa madai ya upande wa Lady Jay Dee hayana mashiko na alimshauri mwanasheria huyo kupitia upya sheria inayozungumzia wanandoa waliotalakiana ili aweze kumshauri vizuri mteja wake kuhusu suala hilo.

Nakala ya barua hiyo pia imetumwa Clouds Media Group na kwa Rais wa Wanafunzi wa Chuo cha TIA.

1 comment:

Anonymous said...

inasikitisha kweli japo kuwa hajamtaja direct lady daydee lakini gardner alimlega yeye.ni nani aliye ishi naye zaidi ya miaka 15 kama si lady jay dee?

wanaumme kama hawa wa design hii ya gardner ni hatari sana wanawake nakupeni ushauri mchunge sana kuwa date na kuolewa na wanaume kama hawa hata kama ana mlungutu wa pesa.utu wenu bora kuliko pesa au umaarufu wa mwanamme.

pole sana lady jay dee mungu atakulipi tuu kuna siku utakuja kuiona.