JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa kuwa kutakuwa na Semina ya wiki moja ya Wakuu wa Kamandi wa majeshi ya Nchi kavu Afrika itakayoendeshwa Mkoani Arusha katika Hoteli ya Mount Meru kuanzia tarehe 13 hadi 19, Mei 2016.
Lengo la Semina hiyo ni kuwakutanisha Wakuu wa kamandi hizo Afrika ili kujadili na kuendeleza ushirikiano katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo mbalimbali yanayolikabili bara la Afrika katika Nyanja ya ulinzi.
Kauli Mbiu ya Semina hiyo ni Ujenzi wa Usalama Afrika kupitia Ushirikiano.
Semina hii hufanyika kila mwaka katika mojawapo ya nchi za Afrika, ili kuwajengea makamanda hao ushirikiano katika kutatua changamoto mbalimbali za kiulinzi zinazotokana na mabadiliko katika Nyanja za kiusalama.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
No comments:
Post a Comment