ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, May 19, 2016

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AWASILI JIJINI MBEYA TAYARI KWA KUFUNGA MAFUNZO YA UONGOZI DARAJA LA PILI KWA MAAFISA WA JESHI LA MAGEREZA

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(katikati) akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Songwe, Jijini Mbeya akiwa ameongozana na Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(kulia). Kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Winifrida Korroso. Katibu Mkuu anatarajia kesho Mei 20, 2016 kufunga Mafunzo ya Uongozi Daraja la Pili kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo cha Magereza Kiwira, Mbeya.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akisalimiana na baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza kutoka vituo mbalimbali vya Magereza Mkoani Mbeya mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Songwe(wa pili kulia) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Camir Minja.

No comments: