ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, May 28, 2016

MBUNGE ATAKA UCHIMBAJI MAFUTA USITISHWE

 Mbunge wa Temeke (CUF), Abdallah Mtolea ameibana Serikali akiitaka kusitisha uchimbaji wa mafuta kwa kuwa haijawa na wataalamu wa kutosha.
Mtolea alitoa kauli hiyo katika swali la nyongeza ambapo alihoji ni kwa nini Serikali ilitangaza kuanza uchimbaji wa mafuta wakati hakuna wataalamu waliozalishwa na vyuo vya ndani.
Katika swali la msingi mbunge huyo alitaka kujua ni lini Serikali itawezesha Chuo cha DMI (Dar es Salaam Maritime Institute) kianze kutoa kazi ya uchimbaji wa mafuta ili wananchi waweze kupata ujuzi na kuajiriwa.
Hata hivyo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani amepinga kauli hiyo akisema kuwa hata kabla ya kuanzishwa kwa chuo hicho tayari Serikali ilishaandaa vijana wengi.
Ngonyani amesema Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) pamoja na Chuo cha Madini cha Dodoma pia, vilishaanza kutoa wahitimu na wako sokoni kwa sas,a hivyo kuanzishwa kwa DMI ni kuongeza idadi ya nafasi.

No comments: