Advertisements

Thursday, May 5, 2016

MWANASHERIA MKUU WA MANISPAA YA KINONDONI ‘ATUMBULIWA’

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mheshimiwa Boniface Jacob akiongea na waandishi wa habari

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mheshimiwa Boniface Jacob ametangaza kumsimamsha kazi mwanasheria mkuu wa manispaa hiyo, Burton Mahenge na Mthamini wa Manispaa Einhard Chidaga.
Uamuzi huo umechukuliwa kwa kauli moja na madiwani wa manispaa hiyo kufuatia kikao chao mwishoni mwa mwezi uliopita.
Mheshimiwa Jacob amewaeleza waandishi wa habari kuwa wawili hao wameisababishia hasara kubwa, kupoteza mali, na kuchelewa kupata manufaa katika mali zake.
Makosa yaliyogundulika katika mashauri hayo ni:
1. Mradi wa uwekezaji wa Oysterbay Villa
Manispaa vilipaswa kupata shilingi milioni 900 kwa mwaka kwa uwekezaji huo. Lakini kutokana na mgogoro wa kimkataba mapato hayajawahi kulipwa hivyo kupoteza shilingi bilioni 4.5 mpaka sasa.

2. Mgogoro wa wapangaji wa nyumba za Magomeni Kota
Manispaa iliandaa mpango wa kuendeleza eneo la Magomeni Kota, hivyo kuwaondoa wapangaji hao na kubomoa nyumba hizo longer, wapangaji walifungua shauri la kupinga kuondolewa katika nyumba na kutoa madai ya kujengewa nyumba ama kulipwa fedha za fidia kutokana na Usimamizi hafifu wa shauri hili Mahakama imeruhusu iliamuru Manispaa kukaa na kumalizana na wapangaji nje ya mahakama. Halmashauri ikatengeneza mkataba wa kuwalipa wapangaji kiasi cha shilingi 1,080,000/= kwa kila mpangaji kama kodi ya mwaka na kumpatia kila mpangaji kiwanja. Hivyo Manispaa inatakiwa kulipa shilingi 3,271,520,000/= kugharamia fidia hiyo kwa mchanganuo wa shilingi 695,520,000/= pango la mwaka na 2,576,000,000/= fidia ya viwanja 644.
3.Uwekezaji eneo la Coco Beach Oysterbay
Manispaa iliingia mkataba na Q – Consult Limited, Kampuni hiyo ilishindwa kutekelezwa mradi kwa wakati na Manispaa ikavunja Mkataba huo. Q-Consult Limited ilifungua shauri ambalo halikusimamiwa vizuri na kwa sababu ya kutofika kwenye kesi, Manispaa ilipoteza kesi hiyo. Halmashauri iliagiza kukata kwa rufaa lakini haikuwa na hatua zozote zilizochukuliwa na hivyo Manispaa inaweza kupoteza haki yake. Iliagizwa na Serikali Mwanasheria Mkuu baada ya tamko la Rais Mhe. John Pombe Magufuli kutangaza nia ya kutoachia eneo hilo mpaka sasa Mwanasheria alikuwa hajakata rufaa.
4.Mradi wa Ujenzi wa maduka Makumbusho (Eastern Capital Ltd)
Mkataba juu ya uendeshaji wa stendi haina manufaa kwa Halmashauri ,KMC inapata 1% ya makusanyo kwa mwaka sawa na Shilingi Milioni 4 tu kwa mwaka, wakati kabla ya uwekezaji, local standy Halmashauri ilikuwa ikipata Milioni 12 kwa mwezi.
5. Kubomolewa kwa ofisi ya Kata ya Msasani
Mwananchi ajulikanaye kwa jina la Chacha aliingilia eneo la ofisi ya kata ya Msasani na baadae kuishtaki Manispaa. Usimamizi dhaifu wa shauri hilo kuisababishia mahakama kutoa amri ya kubomoa ofisi ya Kata, Manispaa imekata rufaa na sasa ni muda mrefu shauri halisikilizwi na hakuna ufuatiliaji unaendeleaje. Hata hivyo kwa makusudi Bw. Chacha aliamua kuuza kiwanda hili kwa Lake Oil CO. Limited wakati shauri halijaisha. Manispaa imekosa manufaa mengi kwa kuchelewa kukamilika kwa shauri hilo, yangu upande wa pili ulikataa Jaji, tuna zaidi ya mwaka hatujapangiwa Jaji mwingine na hatujafuatilia kama Halmashauri.
6. Ujenzi wa Nyumba za makazi (Apartment) Hill Road Oysterbay
Mradi unafanyika kwa ubia na mwekezaji Texas Enterprise Company Ltd, mkataba uliingiwa mwaka 2009, na mradi umesimama kwa muda mrefu sasa.Pamefanyika mabadiliko katika mkataba na mkataba umefanyiwa marekebisho bila idhini ya Halmashauri. Manispaa inakosa manufaa ya mali yake kwa sababu ya kuchelewa kwa mradi. Lakini pia uendeshaji mpya wa sasa hauna makubaliano wa Financial proposal na Investment capital.
7. Ujenzi wa Nyumba za makazi (Apartments) Kiwanda no. 314 Toure Drive
Mradi huu unatekelezwa kwa ubia na Kampuni ya Lake Oil Limited mkataba uliingiwa 2009.
Mabadiliko yamefanyika katika Mkataba bila idhini ya Halmashauri na kuisababishia mradi kuchelewa kukamilika, Manispaa inakosa manufaa ya mali yake kwa kuchelewa kukamilika mradi. Halmashauri bado inaendelea kufuatilia miradi mwingine ambayo umeingia na haina manufaa kwa Halmashauri.

No comments: