Advertisements

Sunday, May 29, 2016

NCHI ZILIZONYUMA KIMAENDELEO BADO ZINA SAFARI NDEFU

C:\Users\Stephen\Desktop\IMG_1976 (1).JPG
Afisa Mkuu wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  Bw. Songelael Shilla, akizungumza katika  Mkutano wa Umoja wa Mataifa unaofanya tathimini ya utekelezaji wa Mpango Kazi  kuhusu  Nchi ambazo zimo nyuma kimaendeleo ( LDCs) Mkutano huu wa siku tatu   unafanyika Antalya nchini Uturuki.

NCHI  ZILIZONYUMA KIMAENDELEO BADO   ZINA SAFARI  NDEFU
Na  Mwandishi  Maalum
Mkutano   unaotathimini mafanikio ya utekelezaji wa  Mpango Kazi wa Miaka 10 kuhusu Nchi ambazo zipo nyuma kimaendeleo, ( Istanbul Program of Action for LDCs) unaendelea  huko Antalya, Uturuki, ambapo imeelezwa kwamba nchi hizo 48 zilizomo katika kundi hilo  bado zina safari ndefu.
Baadhi ya  mambo yanayochelewesha   mataifa hayo  ku-graduate ambayo 38 ni kutoka  Bara la Afrika, 13 kutoka  Bara la Asia na moja kutoka  Amerika ya Latini,ni  pamoja na, umaskini uliokidhiri  ambapo asilimia 51 ya idadi ya  watu katika nchi hizo  ni maskini, idadi kubwa ya watoto ( milioni 18) wenye umri wa kwenda shule  hawaendi shule , rushwa,   na ukuaji  wa uchumi.

Mkutano huo wa  siku tatu  umeandaliwa na Umoja wa Mataifa, kwa kushirikiana na  Serikali ya Uturuki  na unafanyika nchini Uturuki ambapo ndipo chimbuko la mpango kazi  huo  uliopitishwa  mwaka 2011. Tanzania  ambayo ni  kati ya nchi 38 kutoka Afrika ambazo  zimokwenye orodha ya  umoja wa Mataifa   kama nchi zilizonyuma kimaendeleo ( LDCs) inashiriki kikamilifu mkutano huo.
Afisa  Mkuu wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,Bw. Songelael Shilla  akizungumza  kwenye mkutano huo  kwa  niaba ya  Tanzania,   pamoja na  mambo  mengine ameelezea jitihada mbalimbali zinazotekelezwa na serikali  ikiwa ni sehemu ya  mikakati yake  ya kuhakikisha kwamba inafunzu  na kuondoka katika kundi   la nchi zilizonyuma kimaendeleo.
Miongoni mwa  juhudi na mikakati  inayofanywa na serikali  ni pamoja na kuhakikisha   inapunguza idadi ya wananchi wake wanaoishi katika umaskini uliopindukia, uboreshaji wa huduma  muhimu  za kijamii,  ambazo ni  afya sambamba na  upunguzaji wa vifo vya watoto wachanga na wanawake wajawazito,, elimu, ujenzi wa makazi  bora, usambazaji wa huduma za maji safi na salama na ujenzi wa miundo mbinu  ikiwamo ya mawasiliano.
Katika  taarifa yake  Tanzania pia imeanisha   mafanikio  kadhaa katika ukuaji wa uchumi wake huku  ikisisitiza haja na umuhimu wa  mataifa  yaliyoendelea kutimiza ahadi zake  katika eneo la misaada ya kimaendeleo  hatua mbayo itasaidia  kuharakisha nchi maskini  kupiga hatua na kuondoka hapo  zilipo
Pamoja na kusisitiza ubia  na ushirikiano kutoka mataifa yaliyoendelea, Tanzania   imesema bado  inaamini kwamba wajibu wa kwanza   wa kuondoka katika  kundi la  nchi maskini  au zilizonyuma kimaendelo  unapashwa kuwa   wa nchi  zenyewe zilizonyuma kimaendeleo.
Tanzania pia imewasilisha  Taarifa yake  ( National  Mid –Term Review  Report) kuhusu utekelezaji wa Mpango  Kazi wa IPoA.

No comments: