Advertisements

Tuesday, May 3, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM MKOANI DODOMA

 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiendesha Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma. Kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kushoto ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein wakifurahia jambo kabla ya kuanza kwa kikao cha cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipowasili mkoani Dodoma kwa ajili ya kikao hicho cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakielekea kwenye kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU.

3 comments:

Anonymous said...

Kwanini viongozi wa Tanzania wanalindwa kupita viongozi WA ulaya ?

Anonymous said...

Kwa sababu muheshimiwa raisi wa kwanza wa Zanzibar mzee Abeid Karume kauliwa kinyama. Sokoine nae tunaimani ni hujuma. Kwame mkrumah nae kauwawa,Patrice Lumumba wa kongo kauwawa, Thomas Sankara kauwawa,nakadhalika nakadhalika sasa waswahili wanasema mjinga anakokwendea siku zote inakuwa shida lakini kwa kurejea anajua. Sasa hayo majipu anayotumbua Magufuli no doubt ameshajijengea maadui wa ndani na nje ya nchi halafu tumuache bila ya ulinzi masuala mengine ya kipumbavu kuulizwa kwani hata Diamond ana walinzi tena wa maana tu.

Anonymous said...

Hahahahahaha!!! Anonymous wa May 3rd, 2016 at 7:58pm umenichekesha sana aiseeee!! Siamini mtu anauliza Eti kwanini viongozi wa Tanzania wanalindwa hivyooo? Kiongozi wa ngazi ya juu Kama Magufuli au Kikwete lazma walindwa maana historian ya marais kuuliwa ni ndefu sana na inajirudia! Kuna wendawazima kila kona kuua Rais Kwao ni sifa!! Na aliekuambia viongozi wa ulaya au marekani au taifa lolote hawalindwi kwa kaasi kubwa ni naniiiii?!?! Ebu fanya utafiti vizuriiii!!!