Sakata la kuhamishwa kwa wafanyabiashara wadogo katikati ya Jiji la Dar es Salaam limeingia mdudu baada ya madiwani wa Ukawa kugomea uamuzi uliotolewa na uongozi wa jiji hilo.
Uamuzi huo ulitolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mngurumi, unadaiwa kutowashirikisha wadau hao na wafanyabiashara wenyewe.
Mwenyekiti wa madiwani wa Ukawa, Manase Mjema mesema Mngurumi ametoa umuzi huo bila pia kumshirikisha hata Meya wa Ilala, Charles Kuyeko.
Wamesema masoko ya Kivule, Tabata Muslim, Ukonga na Kigogo Fresh ambayo yametengwa mkurugenzi huyo amesema yametengwa kwa ajili ya wafanyabiashara hao, hayajaboreshewa miundombinu yake ikiwamo ujenzi wa vyoo na mabomba ya maji.
Wamemtaka kusitisha mchakato huo mpaka watakapo jadiliana tena.
No comments:
Post a Comment