Monday, May 9, 2016

SUMATRA YATANGAZA NAULI YA MABASI YAENDAYO KASI DAR, RUTI NDEFU SH 650

Mkurugenzi wa SUMATRA, Bw. Giliadi Ngewe akionyesga leseni maalum kwa waandishi wa Habari (Hawapo pichani) wakati wa kukabidhi leseni hiyo kwa Mkurugenzi Mkuu wa UDA-RT, Bw. David Mgwassa (Katikati). Kushoto ni Mkuu wa Wakala wa Mabasi haraka (DART), Bw. Ronald Rwakatare. Tukio limefanyika leo Mei 9.2016 jijini Dar e Salaam. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).

Mkurugenzi wa SUMATRA, Bw. Giliadi Ngewe akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo pichani) wakati wa kutangaza nauli hizo za mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Wakala wa Mabasi haraka (DART), Bw. Ronald Rwakatare na kuliwa ni Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri wa Barabara wa Sumatra, Johansen Kahatano.

Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA dakika chache kutoka sasa tayari imetangaza rasmi viwango vya nauli ya mabasi yaendayo kasi Jijini Dar es salaam huku ikitoa leseni kwa kampuni itakayosimamia mabasi hayo.
Akitangaza nauli hizo mpya kwa umma, jijini Dar es Salaam leo Mei 9.2016, Mkurugenzi wa SUMATRA, Bw. Giliadi Ngewe amebainisha kuwa baada ya kupokea maombi na kisha kuyafanyia kazi wamekuja na kiwango hicho cha nauli kutokana na njia zilizopo kwenye barabara za mabasi hayo yaendayo haraka.
Ambapo katika njia hizo kutakuwa na aina Zaidi ya mbili ambazo zitakuwa na tofauti ya ulipaji wake ikiwemo ile ndefu ambayo ni (Trunk route) huku ile ndogo itakuwa ni (Feeder route ) ama (Trunk+Feeder route).
Kwa upande wa njia ya FEEDER kwa njia fupi ni kwa abiria wanaotoka Mbezi Mwisho kwenda Kimara ambapo nauli itakuwa ni Tsh. 400 kwa mtu mzima na Wanafunzi itakuwa ni Tsh. 200. Hii ni hivyo hivyo kutoka Kimara kwenda Mbezi mwisho.
Kwa upande wa njia TRUNK- nauli itakuwa ni Tsh. 650 ni ile inayozihusisha njia za:

Kimara-Kivukoni/Kivukoni Kimara

Kimara-Kariakoo/Kariakoo-Kimara

Kimara –Morocco/Moroco-Kimara

Moroko-Kivukoni/Kivukoni-Morocco

Morocco-Kariakoo/Kariakoo-Morocco

Kariakoo-Kivukoni/Kivukoni-Kariakoo


Kwa upande wa njia za FEEDER+ TRUNK- Nauli kwa njia hizi itakuwa ni TSH. 800 ni ile inayozihusisha njia za:

Mbezi Mwisho-Kimara-Kivukoni/Kivukoni-Kimara-MbeziMwisho
Mbezi Mwisho-Kimara-Kariakoo/Kariakoo-Kimara -Mbezi Mwisho
Mbezi Mwisho-Kimara-Morocco/Morocco-Kimara-Mbezi Mwisho

Aidha, katika tukio hilo, Mkurugenzi wa SUMATRA, Bw. Giliadi Ngewe alikabidhi leseni maalum kwa Mkurugenzi Mkuu wa UDA-RT, Bw. David Mgwassa ambapo alimtaka afanye kazi kwa mujibu wa sharia huku leseni hiyo ikiwa ni yam waka mmoja ambapo itaisha mpaka Mei 8 2017, Hata hivyo alieleza kuwa, UDA wanayo haki ya kuongeza mkataba kadri watakavyoona inafaa.
Aidha, Mabasi hayo siku ya kesho Mei 10 na 11, watatoa ofa ya bure kwa kwa wananchi wote kupanda bure ilikupata elimu elekezi na namna ya uendeshaji. Hivyo wananchi wajitokeze kwa wingi kuyapanda mabasi hayo kama taratibu zitakazowekwa.
Mkuu wa Wakala wa Mabasi haraka (DART), Bw. Ronald Rwakatare akitoa ufafanuzi wa namna walivyojipanga kudhibiti magari mengine ambayo hayaruhusiwi kutumia njia hiyo ya DART. wakati wa mkutano huo wa SUMATRA wa kutangza nauli kwa mabasi yaendayo haraka.

No comments: