ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, May 22, 2016

TAARIFA KUTOKA KWA FAMILIA YA MAREHEMU WILSON KABWE KUFUATIA UPOTOSHWAJI WA BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI

Familia ya Marehemu Wilson Kabwe  imesikitishwa sana na taarifa zilizosambazwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu kauli na msimamo wa familia katika shughuli za maazishi ya mpendwa wao Wilson Kabwe.

Familia inapenda kuchukua nafasi hii kutamka bayana kwamba, Dk. Zawadi Machuve si msemaji wa familia. Kauli yake iliyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba:-


" Sisi hapa hatukaribishi viongozi, huu ni msimamo wa familia kama wao watafanya utaratibu wao sawa, lakini hatuko kwa ajili ya viongozi"



Kauli hiyo ambayo ililenga kutoishirikisha Serikali katika msiba wa mtumishi wake tunaomba ipuuzwe na siyo kauli ya familia.


Familia inatambua na inathamini sana mchango mkubwa wa Serikali katika kugharamia matibabu na  huduma  zote za mazishi.


Familia inachukua fursa hii kuwakaribisha viongozi wote wa Serikali, ndugu, jamaa na marafiki wanaopenda kushiriki katika shughuli za mazishi ya mpendwa wetu.

Imetolewa na:

PHILIP MKENGA KABWE

MSEMAJI WA FAMILIA.

No comments: