Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imegawa Sukari yote ya Magendo Mifuko 5319 yenye thamani ya Zaidi ya Shilingi Million 373.5 kwa Taasisi mbali mbali Mkoani Lindi baada ya kuthibitishwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA kuwa ni Salama kwa matumizi ya binadamu.
Sukari hiyo ilikamatwa mwezi Februari mwaka huu katika bandari ya Lindi ndani ya meli ya MV Hassanat ikiingizwa kinyume cha Sheria ikitokea nchini Brazil kupitia Zanzibar.
Sukari hiyo ilipaswa kulipiwa Kodi zaidi ya shilingi Million 246.
Akizungumza wakati wa ugawaji wa sukari hiyo mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipakodi - TRA Bw Richard Kayombo alisema baada ya kukamatwa kwa bidhaa hizo, TRA kwa kushirikiana na taasisi nyingine za serikali akiwemo mkuu wa mkoa wa lindi waliamua kuigawa sukari hiyokwa watuwenye uhitaji katika mkoa wa Lindi pamoja na wilaya zake.
Aidha Bw. Kayombo alitoa wito kwa watu wote wanaofanya biashara za magendo, haramu na ukwepaji kodi kuacha mara moja kwani sasa TRA ina mikakati thabiti na endelevu ya kudhibiti biashara za magendo pamoja na ukwepaji kodi kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment